Skip to main content

RC CHALAMILA AWATAKA WATANZANIA KUDUMISHA AMANI NA KUWAENZI MASHUJAA



Na Mwandishi wetu, HabariPlus

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amewataka watanzania kuendelea kudumisha amani na utulivu katika jiji hilo, huku akiwataka kuwaenzi mashujaa wa Tanzania waliopigania uhuru wa taifa hilo.

Rai hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam wakati alipokua katika maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya mashujaa wa Tanzania katika eneo la mnara wa mashujaa mnazi Mmojq ilala jijini Dar es Salaam.

Aidha RC Chalamila amesema siku ya mashujaa ina umuhimu mkubwa katika historia ya Tanzania na kusema kuwa njia bora ya kuwaenzi mashujaa hao ni kuendelea kudumisha Amani na kuepuka viashiria vyote vya uvunjifu wa amani.

Amesema kuwa,  muasisi wa Taifa la Tanzania Hayyt Mwl Julius K Nyerere na Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayyat Abeid Karume hao wamekua mfano mzuri wa kuigwa kila inapoazimishwa siku ya mashujaa kwani amani iliyopo imetokana na misingi imara walioiweka.

"Kila ifikapo Julai 25 tunaadhimisha siku hii kwa kuwakumbuka wapigania uhuru mbalimbali wa taifa hili, wapo wengi ambao wengine wamekufa na wengine wapo hai wamefanya makubwa nchi hii "amesema RC Chalamila.

Ameongeza kuwa, wako mfano mzuri wa mashujaa  walio hai ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ni shujaa aliye hai kupitia kazi nzuri anayoifanya ndani ya Taifa hili ikiwemo utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo katika jamii kama vile SGR, Bwawa la Mwl Nyerere na miradi mingine mingi ya Elimu na Afya.

Aidha, uhuru ulipo katika nchi hiyo ni ishara ya watu ambao wameacha alama kwa sababu ya uzalendo na ushajaa waliouonesha kwa kujitoa kwa nchi yao kuhakikisha inapata amani na inakua na uhuru ambapo mashujaa wengi wamerithi.

"Tunapozungumzia mashujaa tunapaswa kulinda na kuepuka na rushwa na fitna na yote yatakayopelekea kubomoka kwa jamii yetu tuendelee kulinda amani na kuenzi uhuru wetu"amesema Chalamila.

Amesema kuwa, Tanzania imepitia majaribu mengi kabla ya kupatikana kwa Uhuru na amani iliyopo sasa na kueleza kuwa Amani iliyopo ni matokeo ya kazi nzuri iliiyofanywa na mashujaa waliopoteza maisha pamoja na mashujaa waliohai ambao ni viongozi waliojitoa kuilinda na kusimamia amani ya nchi , hivyo ni muhimu kila mtu kuilinda amani.

Katika hatua nyengine Rc Chalamila amewataka watanzania kuendelea kuliombea taifa la Kenya kutokana na hali wanayopitia  kwani ushajaa ni amani bila amani nchi haiwezi kuwa salama.

Ifahamike kuwa maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya mashujaa Kitaifa yamefanyika katika Mkoa  wa Dodoma ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassani ameongoza maadhimisho hayo.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...