Skip to main content

AJALI YA TRENI KIGOMA TRC YATOA TAMKO



Na Mwandishi wetu, Kigoma 

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli nchini (TRC) Masanja Kadogosa  ametembelea majeruhi wa  ajali ya treni mkoani Kigoma na kusema Serikali  itagharamia matibabu ya abiria 73 waliojeruhiwa katika ajali ya treni ya abiria iliyoanguka eneo la Lugufu wilaya ya Uvinza usiku wa kuamkia Agosti 28 mwaka huu.

Kadogosa amesema  hayo  alipowatembelea majeruhi katika hospitali ya rufaa ya mkoa kigoma Maweni na hospitali ya wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma ambapo amesema kuwa pamoja na kugharamia matibabu kwa majeruhi wote pia TRC itawasafirisha majeruhi wote wa ajali hiyo kuendelea na safari zao hadi wanapokwenda.

 Akiwa hospitali ya rufaa ya mkoa Kigoma Maweni Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk.Lameck Mdengo amesema kuwa hadi sasa wamebaki wagonjwa wanne kati ya watano waliokuwa wamelazwa hospitalini hapo.

Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa hospitali ya wilaya Uvinza, Dk.David Patrick George alisema kuwa wagonjwa 73 walipokewa hospitalini hapo siku ya ajali na hadi kufikia leo mchana wakati Mkurugenzi Mkuu anatembelea majeruhi hospitalini hapo walibaki wagonjwa sita ambapo  katika wagonjwa hao  watatu waliomba kuendelea na safari baada ya ziara ya Mkurugenzi Mkuu hospitalini hapo na wagonjwa watatu watahamishiwa hospitali ya rufaa ya mkoa Kigoma Maweni kwa matibabu zaidi.

Baadhi ya wagonjwa waliolazwa katika hospitali za rufaa mkoa Kigoma akiwemo Hamida Hamza ambaye ameumia mgongo na mbavu amelishukuru shirika la reli, uongozi wa serikali ya mkoa na waganga katika hospitali za Uvinza na kwa jitihada kubwa walizofanya tangu ajali ilipotokea hadi sasa wanapoendelea na matibabu ambapo hawajadaiwa gharama zozote za matibabu wala chakula.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...