Skip to main content

OFISI YA MAKAMO WA RAIS MUUNGANO NA MAZINGIRA YAANDA MKUTANO WA KUJADILI CHANGAMOTO ZA MAZINGIRA

 

Na Mwandishi wetu, Dar 

Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira imepanga kukutana na viongozi, wataalamu na wadau wa Mazingira na mabadiliko ya tabianchi kwa lengo la kujadili na kuweka mikakati ya kujadili changamoto za mazingira.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Waziri wa Nchi ofisi ya makamo wa Rais Muungano na Mazingira Dkt Ashantu Kijaji amesema kuwa mkutano huo utafanyika Septemba 09 hadi 10 , 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma ambapo mawasilisho mbali mbali yatatolewa ikiwa ni pamoja na usimamizi wa taka, nishati safi na .

Amesema kuwa,  kumekuepo na changamoto mbalimbali za mazingira ambazo zinafifisha ustawi wa jamii na uchumi, ikiwa ni pamoja uharibifu wa ardhi, vyanzo ya maji, ukataji miti ovyo na uharibifu wa misitu.

Aidha amesema kuwa Mazingira na Maliasili ni msingi wa uhai wa binadamu , hivyo usimamizi na hifadhi ya rasilimali hizo ni suala la kipaumbele na lenye umuhimu wa kipekee. 

Hata hivyo, amesema kuwa changamoto za uharibifu wa mazingira unasababisha upotevu wa makazi ya wanyamapori na bayoanuai, athari za mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa mifumo-ikolojia ya pwani na baharini, uharibifu wa ardhi oevu, uchafuzi wa mazingira na kuenea kwa viumbe vamizi.

"Changamoto hizi zinachangiwa na shughuli za binadamu zisizo endelevu ikiwemo utegemezi mkubwa wa kuni na mkaa kama chanzo cha nishati, kilimo kisicho endelevu, utupaji taka ovyo na ufugaji wa mifugo usiowiana na maeneo ya malisho"amesema Dkt Kijaji.

Ameongeza kuwa "Changamoto nilizozitaja hapo awali zinaathiri sekta muhimu za uchumi kama vile kilimo, nishati, maji, uvuvi na utalii; ustawi wa jamii na viumbe hai, hivyo, kwa kutambua mchango wa wadau katika kuhifadhi na kusimamia mazingira na mabadiliko ya tabianchi nchini"

Amesema kuwa mkutano huo unalenga kuimarisha uwajibikaji, ufanisi na usimamizi wa hifadhi ya mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. 

Ameongeza kuwa Mkutano huo unatarajia kushirikisha wadau zaidi ya 1,000 kutoka katika Wizara na Taasisi za Serikali, Mashirika ya Umma, Sekta binafsi, vyuo vya elimu ya juu na Asasi zisizo za Serikali. 

"Viongozi watakaoshiriki Mkutano huu ni Mawaziri na Makatibu Wakuu kutoka Wizara za Kisekta, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, na Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Tanzania Bara Vile vile, Mkutano utashirikisha Wakurugenzi kutoka katika mashirika ya Umma na wataalamu; Sekta Binafsi; na Asasi zisizo za kiserikali." 

Aidha amesema kuwa Mkutano huo utajadili fursa zilizopo katika hifadhi na usimamizi wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi. Hii ni pamoja na Biashara ya Kaboni, usimamizi wa taka, mabadiliko ya tabianchi,  nishati safi ya kupikia, upandaji miti na usimamizi na uzingatiaji wa Sheria nchini.

Hata hivyo, Waziri Ashantu Kijaji amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa jitihada anazofanya kuimarisha hifadhi na usimamizi wa mazingira nchini.

"Mheshimiwa Rais ameendelea kusimamia na kutoa mwongozo mahsusi katika kuhakikisha kuwa mazingira na maliasili zinahifadhiwa na kuongeza mchango katika Pato la Taifa.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...