Skip to main content

RAIS DKT SAMIA KUHUTUBIA JUKWAA LA FOCAC, TAZARA KUFUFULIWA UPYA

Na Mwandishi wetu,Dar

Rais wa Jamhuri wa Muungano Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuongoza Ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa Kilele wa wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika utakaofanyika kuanzia tarehe 4 hadi 6 Septemba 2024 jijini Beijing, China.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Thabit Kombo (MB) amesema kuwa Dkt Samia anashiriki mkutano huo kufuatia mwaliko wa  Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Xi Jinping.

Amesema kuwa, ushiriki wa RAIS DKT Samia kwenye mkutano wa kilele wa FOCAC umelenga kuendelea kudumisha ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na China ambao mwaka huu umetimiza miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili.

 Pia kujadiliana na kukubaliana na Serikali ya China namna ya kuendelea kuongeza ushirikiano katika maeneo ya kipaumbele kwa maendeleo ya pande ya Taifa ikiwemo katika sekta ya miundombinu, mifumo ya chakula, biashara na uwekezaji, kubadilishana ujuzi, upatikanaji wa nishati safi na salama na kusaidia ujenzi wa uchumi wa kidijitali. 

Ameongeza kuwa, pia kuibua fursa mpya za ushirikiano kwa manufaa ya pande zote mbili pamoja na kutangaza maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya Sita ya sera na sheria katika sekta ya biashara na uwekezaji ili kuvutia wawekezaji wengi zaidi kutoka nchini humo.

Aidha, Serikali ya China imemteua Rais Dkt. Samia kuhutubia kwenye hafla ya ufunguzi wa mkutano huo wa Kilele wa wakuu wa Nchi na Serikali wa FOCAC itakayofanyika tarehe Septemba 4 hadi 6, 2024, akiiwakilisha Kanda ya Afrika Mashariki, huku kauli mbiu ikiwa “Kushirikiana ili Kuendeleza Usasa na Kujenga Jamii Bora ya China na Afrika kwa Mustakabali wa Pamoja"

Amesema kuwa, ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo utaongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ataungana na wakuu wa Nchi na Serikali wenzake kutoka Nchi zaidi ya 40 kati ya 54 za Bara la Afrika kushiriki Mkutano huo.

Amefafanua kuwa jukwaa la FOCAC lilianzishwa mwaka 2000 na Jamhuri ya watu wa China kwa lengo la kukuza ushirikiano na maendeleo ya pamoja kati ya China na Afrika,  ambapo tangu kuanzishwa kwake jumla ya mikutano ya Kilele (Wakuu wa Nchi na Serikali) nane (8) imefanyika.

"Mikutano hiyo hufanyika kila baada ya miaka mitatu kwa kubalishana kati ya China na nchi moja ya Afrika, mkutano huu wa 9 wa FOCAC utafungulia na Xi Jinping, Rais wa Jamhuri ya Watu wa China ambapo, hotuba yake ya ufunguzi itatoa uelekeo wa China katika uhusiano wake na nchi za Afrika, 

Aidha, viongozi mbalimbali watashiriki katika mkutano huo ikiwa ni pamoja na Antonia Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Moussa Faki, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika watashiriki Mkutano huo.

Hata hivyo, amesema mada zitakazojadiliwa ni pamoja na Utawala wa Nchi, Mpango wa Miundombinu na Uwekezaji, Maendeleo ya Viwanda na Kilimo cha Kisasa na Amani na Usalama, kwa upande wa Tanzania utajikita kwenye mada ya Maendeleo ya Viwanda na Kilimo cha Kisasa mada hiyo imezingatia Mpango wa Maendeleo wa Tatu wa Miaka Mitano, ambao ndiyo mpango wa mwisho wa utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Tanzania ya 2025.

Hata hivyo, Tanzania inatarajia kuwasilisha miradi mbalimbali ikiwemo mipya na ile ambayo haiweza kutelezwa kwenye mpango uliopita wa FOCAC kwa sababu mbalimbali, ili iweze kutekelezwa chini ya Mpango Kazi wa FOCAC kwa kipindi cha 2025-2027 kwa kupatiwa fedha za mkopo nafuu na msaada.

 Miradi hiyo ni pamoja na Ujenzi wa Mtandao wa Mawasiliano Vijijini wa awamu ya Pili, ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa Kv 400 wa awamu ya Pili na Tatu , Ujenzi wa Vyuo vya Ufundi Stadi (VETA) wa awamu ya Pili na Ujenzi wa Babara za Zanzibar Zenye Urefu wa Kilomita 277.7 .

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...