Skip to main content

TAWA YATIA SAINI MIKATABA YA UWEKEZAJI WA MIUNDOMBINU YA UTALII

YATARAJIA KUIINGIZIA SERIKALI ZAIDI YA BILIONI 27 KWA MWAKA

ipline, Loji zenye hadhi ya nyota 5 na Kambi za Kitalii zenye hadhi ya nyota 4 kujengwa

Na. Beatus Maganja 

MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA leo Agosti 24, 2024 imetia saini mikataba minne (4) ya uwekezaji wa miundombinu ya utalii na kampuni za Sea and Bush Ltd na  Ritungu Tours and Safaris Ltd Katika mapori ya Akiba ya Kijereshi, Pande na Swagaswaga na eneo la Makuyuni.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mikataba hiyo iliyofanyika  kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TAWA Mej. Jen. (Mstaafu) Hamis R. Semfuko amesema kusainiwa kwa mikataba hiyo ni sehemu ya jitahada za TAWA katika kuunga mkono kwa vitendo maono ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kukuza na kuendeleza biashara ya utalii nchini.

Semfuko amesema kupitia uwekezaji huo, TAWA inatarajia kuingizia Serikali mapato ya wastani wa Shillingi Bilioni 27.3 kwa mwaka. Aidha, amesisitiza kuwa Bodi yake imejipanga kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa mikataba hiyo ili kuleta tija iliyokusudiwa katika kukuza utalii na uwekezaji katika tasnia ya utalii nchini.

Aidha, Mwenyekiti huyo ameahidi kuwa Bodi yake itawapa ushirikiano stahiki wawekezaji wote ili kuhakikisha wanafikia malengo yao ya uwekezaji katika maeneo yanayosimamiwa na TAWA.

 Vilevile, Semfuko amesema kuwa Bodi ya Wakurugenzi ya TAWA ina matarajio ya kuona uwekezaji huo ukisaidia kuboresha miundombinu ya utalii, kutoa ajira kwa watanzania  na kuboresha maisha ya jamii inayozunguka maeneo ya uwekezaji ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea katika maeneo hayo ili kujionea vivutio vilivyopo na kuongeza mapato ya Serikali.

Kwa upande wake Kamishna wa Uhifadhi wa TAWA, Mabula Misungwi Nyanda amesema katika kuhakikisha kuwa maeneo yanayosimamiwa na Taasisi hiyo yanaongezewa thamani  katika kipindi cha mwaka wa fedha 2023/24, TAWA ilitangaza kwa umma fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo katika maeneo yake na kupata jumla ya maombi matano kutoka kwa Kampuni 3 zilizoomba kuwekeza katika maeneo hayo.

Amesema hatua hiyo ililenga kufikia malengo ya Serikali ya kuongeza idadi ya watalii kutoka millioni 1.5 hadi watalii millioni 5 na mapato kutoka dola za Marekani bilioni 2.6 hadi bilioni 6 kwa mujibu wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya Mwaka 2020/2025.

Sanjari na hilo, Kamishna Mabula amesema uwekezaji na kampuni hizo utakuza Utalii kwa kuongeza idadi ya vitanda katika maeneo yanayosimamiwa na TAWA ambapo jumla ya vitanda 360 vitaongezwa na wawekezaji katika maeneo ya uwekezaji kwa kujenga Loji zenye hadhi ya nyota 5 na Kambi za kitalii zenye hadhi ya nyota 4 katika Pori la Akiba Kijereshi na Hifadhi ya Wanyamapori ya Makuyuni na kuanzishwa kwa zao jipya la utalii aina ya "Zipline" katika Pori la Akiba Pande ili kuchochea na kukuza utalii Katika Jiji la Dar es Salaam.

Ujenzi wa Loji na Kambi za Kitalii katika Pori la Akiba Kijereshi (Simiyu) na Hifadhi ya Makuyuni Wildlife Park (Arusha) utafanywa na Kampuni ya Sea and Bush Ltd , huku kujengaa na kuendesha Zipline katika Pori la Akiba Pande (Dar es Salaam) na ukodishaji na uendeshaji wa Hosteli ya Pori la Akiba Swagaswaga (Dodoma) ukitarajiwa kufanywa na Kampuni ya Ritungu Tours and Safaris Ltd.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...