Skip to main content

TMA YAWANOA WATAALAM WA HALI YA HEWA BARANI AFRIKA


Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mnyaa Mbarawa (Mb) akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kuwajengea uwezo wataalamu wa hali ya hewa kutoka Taasisi za Hali ya Hewa barani Afrika, Kitengo cha Elimu na Mafunzo cha Shirika la Hali ya Hewa Duniani kwa kushirikiana na Chuo cha Taifa cha Hali ya Hewa kinachoendeshwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Mwakilikishi kutoka WMO (Ofisi ya Mafunzo), Bi. Eunjin CHOI akifafanua jambo katika wa mafunzo kuwajengea uwezo wataalamu wa hali ya hewa kutoka Taasisi za Hali ya Hewa barani Afrika, Kitengo cha Elimu na Mafunzo cha Shirika la Hali ya Hewa Duniani kwa kushirikiana na Chuo cha Taifa cha Hali ya Hewa kinachoendeshwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Mwakilishi wa kudumu wa WMO, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hew ana Tabianchi, Dkt. Ladislaus Chang’a akizungumza wa mafunzo kuwajengea uwezo wataalamu wa hali ya hewa kutoka Taasisi za Hali ya Hewa barani Afrika, Kitengo cha Elimu na Mafunzo cha Shirika la Hali ya Hewa Duniani kwa kushirikiana na Chuo cha Taifa cha Hali ya Hewa kinachoendeshwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Mwanza
Katika kuwajengea uwezo wataalamu wa hali ya hewa kutoka Taasisi za Hali ya Hewa barani Afrika, Kitengo cha Elimu na Mafunzo cha Shirika la Hali ya Hewa Duniani kwa kushirikiana na Chuo cha Taifa cha Hali ya Hewa kinachoendeshwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), wameandaa mafunzo mahsusi ya matumizi ya data na taarifa za Rada za Hali ya Hewa. Mafunzo hayo yanafanyika katika Ukumbi wa Malaika,Mwanza, tarehe 26 hadi 30 Agosti 2024.

Akifungua rasmi mafunzo hayo, Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mnyaa Mbarawa (Mb); alieleza lengo la mafunzo hayo ni kuimarisha zaidi uwezo wa wataalamu wa hali ya hewa na wataalam wengine husika kutoka baadhi ya Nchi za Afika Mashariki na Kusini mwa Afrika katika matumizi bora ya taarifa za Rada za hali ya hewa kwa ajili ya kuboresha utabiri wa hali ya hewa na utoaji wa tahadhari za matukio ya hali mbaya ya hewa kwa jamii.
Aidha, alieleza kuwa mafunzo hayo yanaendana na utekelezaji wa mpango ulioasisiwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa utoaji wa Tahadhari kwa Wote (Early Warning for All EW4ALL) ifikapo mwishoni mwa mwaka 2027, pamoja na Sera ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) ya ubadilishanaji wa data za hali ya hewa Kimataifa (“WMO Unified Data Policy”). Mafunzo hayo yana umuhimu mkubwa kwa nchi wanachama wa WMO kanda ya Afrika (WMO RA1) katika kuongeza uwezo unaohitajika zaidi wa utoaji wa huduma za hali ya hewa na tahadhari kupitia taasisi za hali ya hewa za nchi husika kukabiliana na ongezeko la idadi na ukubwa wa matukio ya hali mbaya ya hewa katika muktadha wa mabadiliko ya hali ya hewa na hivyo kuchangia kuokoa maisha ya watu na mali zao.

Alisisitiza umuhimu wa kufanya uwekezaji wa miundo mbinu ya kisasa ya hali ya hewa kama vile rada, akifafanua kuwa Tanzania imekuwa kilelezo bora katika kufanya uwekezaji huo pamoja na kuwajengea uwezo wataalamu wa hali ya hewa nchini, na hivyo kuchochea fursa ya kuandaa mafunzo hayo.

Awali, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Mwakilishi wa kudumu wa WMO, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hew ana Tabianchi, Dkt. Ladislaus Chang’a, alieleza kuwa TMA imejiandaa vyema kupitia wataalamu wake katika kutoa mafunzo hayo “Wataalamu watakao toa mafunzo ni wabobezi, na kati yao wamepata mafunzo kutoka Marekani na Finland na vilevile ni wakufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam”. Alisema Dkt. Chang’a.

Kwa upande wake, Mwakilikishi kutoka WMO (Ofisi ya Mafunzo), Bi. Eunjin CHOI aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa kufanikisha mafunzo hayo muhimu ya matumizi ya taarifa na data za rada za hali ya hewa. “Kupitia ushirikiano huu, kwa pamoja tunaweza kuendeleza malengo yetu ya kuboresha huduma za hali ya hewa, si tu kwa Tanzania bali duniani kote”. Alisisitiza Bi. Eunjin.

Tanzania inatoa mafunzo kwa wataalamu wa hali ya hewa kutoka baadhi ya nchi Wanachama wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) kanda ya Afrika ambao ni Burundi, Comoro, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya, Msumbiji, Malawi, Mauritius, Rwanda, Seychelles, Sudan Kusini, Uganda, Tanzania na Zambia.


Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...