Skip to main content

UWEPO WA TAWA WAONGEZA HADHI YA TAMASHA LA KIZIMKAZI - SALIM KIKEKE


Na. Beatus Maganja

Mtangazaji nguli, na mwandishi wa habari mashuhuri Africa Mashariki na Kati aliyekuwa akitangaza kipindi cha Dira ya Dunia katika Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) ambaye kwasasa anafanya kazi  na Redio/TV ya Crown  FM/TV iliyopo nchini, Salim Kikeke amesema uwepo wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini - TAWA katika Tamasha la Kizimkazi umekuwa chachu ya kuchagiza na kulipa hadhi tamasha hilo kutokana na Taasisi hiyo kuwapeleka wanyamapori hai ambao wamekuwa kivutio kikubwa kwa watalii wengi wanaotembelea banda la Wizara ya Maliasili na Utalii.

Kikeke ameyasema hayo leo Agosti 21, 2024 alipotembelea banda la Wizara ya Maliasili na Utalii na kufika katika bustani ya wanyamapori hai ambapo alipata fursa ya kujionea aina mbalimbali za wanyamapori wakiwemo Simba, Chui, Fisi, Chatu, Pundamilia na spishi za aina tofauti za ndege nyuni.

"Niko hapa Kizimkazi kwa ajili ya Tamasha la Kizimkazi na nimefurahi sana kutembelea banda hili la TAWA...kuna mabanda mengi sana lakini TAWA wameweza kuleta kivutio cha kipekee kabisa, wameleta wanyama mbalimbali na zaidi ni kuonesha hazina ya Taifa letu" amesema

"Nadhani kitu TAWA wanakifanya ni muhimu sana kuweza kuja kutoa elimu na kufahamisha jamii yetu ya hapa hapa nyumbani lakini vilevile watu wanaotoka nje  ya Taifa letu kufahamu maana halisi ya wanyama hawa, jinsi tunavyowatunza na jinsi wanavyolisaidia Taifa letu kwa njia ya kipato kwahiyo pongezi nyingi sana kwa TAWA kwa kile wanachokifanya uwepo wao nadhani umeongeza ile hadhi ya Kizimkazi" ameongeza na kusisitiza Kikeke

TAWA ni mojawapo ya Taasisi za Serikali zinazoshiriki katika Tamasha hilo   kwa lengo la kutangaza fursa za utalii zilizopo katika maeneo yake ya kimkakati yaliyo chini ya usimamizi wake hususani ya ukanda wa Kusini Mashariki Kama vile Hifadhi za Selous, Kilwa, Pande (Dar es Salaam), Wamimbiki (Pwani/Morogoro) n.k ikiwa ni muendelezo wa kuunga mkono jitahada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alipotangaza vivutio vya Utalii wa nchi yetu kupitia filamu Maarufu za Tanzania The Royal Tour na Amazing Tanzania.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...