Skip to main content

KIKOSI CHA AFYA JESHI LA POLISI KIMEZINDUA KAMPENI YA KUPIMA AFYA BURE KATIKA MAADHIMISHO YA WIKI YA POLISI

 


KAMISHNA Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) Abdallah Mpallo amesema jamii ijitokeze kupima afya  kwenye kambi zinazokuwa kimeandaliwa ili kuikomboa afya na magonjwa yanayoambukiza na yasiyoambukiza.

Mpallo ambaye pia anatoka kikosi cha afya alisema katika kuelekea kilele cha wiki ya Polisi shughuli mbalimbali zimefanyika ikiwa ni pamoja na kutoa huduma za Afya kwa kupima magojwa mbalimbali.

Mpallo alisema hayo leo Septemba 11, 2024 wakati akimuwakilisha Kamanda wa Kikosi cha Afya Naibu Kamishna wa Polisi, DCP Lucas Mkondya.

"sisi kama kikosi cha polisi tumelenga kutoa huduma za vipimo bure kwa watu wote ili kutambua afya zao na endapo mtu atagundulika kuwa anahitaji matibabu makubwa zaidi atapewa rufaa ya kwenda hospitali kubwa ilikuendelea na matibabu zaidi. Pia tunatoa elimu kuhusu magonjwa yanayoambukiza na yasiyoambukiza hasa namna ya kijikinga na homa ya nyani (Mpox).

ACP. Mpallo alisema katika kambi hiyo itatolewa elimu hukusu mguu kifundo kwani watu wengi uamini kuwa ulemavu huo unasababishwa na imani za kishirikina.

"Kikosi cha Afya kitatoa elimu juu ya mguu kifundo kwani watoto wengi huzaliwa wakiwa na ulemavu huo lakini wazazi wao hudhani kuwa hiyo ni laana bali ni mapenzi ya Mungu lakini pia kuna hospitali nyingi ambazo zinafanya upasuaji wa kuondoa mguu kifundo,"alisema.

Mpallo alisema huduma hizo zinatolewa katika hospitali ya mkoa wa kipolisi Kurasini na akatumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kuachana na mila potofu kwani mila hizo zinarudisha maendeleo nyuma huku akiwakaribisha polisi na wananchi wote kushiriki katika maadhimisho hayo.

Maadhimisho ya miaka 60 ya kuzaliwa Polisi yenye kauli mbiu"Elimu ya afya, huduma bora ya kipolisi kwa umma itapatikana kwa kubadilika kifikra, usimamizi wa sheria na matumizi ya tehama"yalianza septemba 2  na yanatarajiwa kuhitimishwa septemba, 13 mwaka huu.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...