Skip to main content

MKURUGENZI WA KAMPUNI YA GREEN HIPPO TRAVEL AZURU MAKUYUNI WILDLIFE PARK

Astaajabishwa na wingi wa vivutio na kuahidi kuwahamasisha wageni mbalimbali kutembelea eneo hilo

Mkurugenzi wa Kampuni mashuhuri  ya utalii inayofahamika kama Green Hippo Travels, Astrid Kleinveld akiwa ameambatana na rafiki yake  Naomi Rugenbrink ambao wote ni raia wa Uholanzi,   tarehe 15 septemba 2024, walitembelea eneo la Makuyuni Wildlife Park liliopo wilayani Monduli mkoani Arusha kujionea vivutio mbalimbali vilivyopo na kupata fursa ya kufahamu namna wanavyoweza kufanya biashara ya utalii katika eneo hili hasa  utalii wa Kupanda Mlima na Kutembea kwa miguu.

Bi Astrid na mwenzake wakiongozwa na Afisa Utalii wa eneo hilo Chacha Masase walipata fursa ya kupanda Mlima Kipara ambao unapatikana ndani ya eneo hilo wenye urefu wa mita 1900 kutoka usawa wa bahari pamoja na kufanya utalii wa Kutembea kwa miguu hivyo kufanikiwa kuona wanyamapori kwa ukaribu zaidi na kufurahia mandhari iliyopo.

"Uzuri wa eneo hili ni wa kustaajabisha mnoo, tumepata uzoefu wa kipekee ambao nina imani sio sisi tu bali mtalii yeyote atakae kuja ataifurahia Makuyuni Wildlife Park kuanzia mapokezi ya wanyamapori tokea njiani, mandhari ya eneo hili,  pamoja na ukarimu na umahiiri wa watumishi wa TAWA" alisema Astrid

" Tumepanda mlima na kutembea kwa miguu tumejionea vivutio vingi ambavyo sasa tunakwenda kuongeza kwenye safari zetu na kuwaalika wageni kutoka pembe zote za dunia kuja kulitembelea eneo hili" aliongeza na  kusisitiza.

Uwepo wa miundombinu wezeshi ya barabara, wingi wa wanyamapori na mandhari ya kuvutia huifanya Makuyuni Wildlife  Park kuwa chaguo bora kwa mtalii yeyote wa ndani na nje ya Tanzania.

Shughuli nyingine za kitalii zinazoweza kufanyika  katika eneo hilo ambalo ni makazi ya wanyamapori mbalimbali wakiwemo Nyati, Simba, Tembo, Chui, Twiga, Pundamilia ni pamoja  na kupanda mlima (Hiking), utalii wa kutembea kwa miguu (Walking Safari),Utalii wa kuona ndege,  kuangalia jua likichomoza na kuzama na  utalii wa Utamaduni (jamii ya kabila la wamasai inayozunguka eneo hili).

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...