Skip to main content

MKUTANO WA 11 WA TAASISI YA MERCK FOUNDATION AFRIKA ASIA LUMINARY KUFANYIKA TANZANIA



Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt.Dorothy Gwajima amesema Taasisi ya uhisani ya Merck Foundation inayojishughulisha na Huduma za Jamii, inatarajia kufanya mkutano wake wa 11 nchini Tanzania tarehe 29 na 30 Oktoba 2024 jijini Dar Es Salaam.

Waziri Dkt. Gwajima ameyasema hayo, akizungumza na Waandishi wa Habari  Septemba 18, 2024 jijini Dar Es Salaam, amebainisha kwamba, Mwenyekiti wa mkutano huo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na kusema, kufanyika kwa Mkutano huo nchini kwa mara ya kwanza, kunatokana na Rais Samia kuridhia ombi la Taasisi hiyo.

Waziri Dkt. Gwajima amesema Taasisi ya Merck Foundation ilipendekeza kufanya Mkutano huo nchini Tanzania kutokana na jitihada za wazi za Serikali, kuwekeza katika sekta ya afya, hasa afya ya akina mama na watoto, ambavyo vimeifanya Tanzania kufanya vizuri katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya kimataifa yakiwemo ya Milenia na Maendeleo Endelevu.

Waziri Dkt. Gwajima ameendelea kusema Mkutano huo unaratibiwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Taasisi ya Merck Foundation na utahudhuriwa na Wenza wa Marais kutoka nchi 22 za Afrika na mwenyeji Tanzania, ambapo Mwenza wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mariam Mwinyi atawakilisha. 

Mkutano utahudhuriwa pia na Mawaziri wa Afya, Jinsia, Mawasiliano, Elimu, Ustawi wa Jamii kutoka nchi zilizoalikwa, Wataalam wa huduma za afya 500, wasomi, watunga sera, Mabalozi, waandishi wa habari na Wajumbe wengine takribani 500 kutoka sehemu mbalimbali za dunia watashiriki kwenye Mkutano kwa njia ya mtandao.

Ameendelea kueleza kuwa, pamoja na mambo mengine mkutano huo utajadili mada nne za kitaalamu kuhusu Afya ya Mama na mtoto, ugonjwa wa Saratani, ugonjwa wa Kisukari na Shinikizo la damu. Mada nyingine ni mafunzo kwa vyombo vya Habari kuhusu Mipango ya Maendeleo na kujengewa uwezo.



Mkutano huo pia utatumika kama jukwaa la kuchukua hatua mahususi katika kushughulikia unyanyapaa na mtazamo wa kijamii wa utasa, kuboresha upatikanaji wa huduma ya uzazi salama iliyodhibitiwa, na yenye ufanisi kwa wanawake na wasichana Barani Afrika.

Waziri Dkt. Gwajima ameongeza kuwa, washiriki wa Mkutano huu watanufaika na maarifa na uzoefu unaotolewa na wataalam mbalimbali na watafiti ambao watazungumza kwa kina kuhusu mada tajwa hapo juu kwa lengo la kuongeza uelewa wa jamii juu ya masuala mbalimbali ya afya ikiwa ni pamoja na Magonjwa yasiyoambukiza, matatizo ya kupumua, na mengineyo.

Aidha, ametoa wito kwa Watanzaniawote kuendelea kudumisha amani, umoja na mshikamano, ambavyo ni tunu za taifa na sumaku kwa wadau mbalimbali wanaofika nchini kwa ajili ya shughuli za utalii, ukiwemo wa mikutano na kujitokeza kuwania fursa mbalimbali zitakazoenda sambamba na uwepo wa wageni katika Mkutano huo.



Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...