Skip to main content

RAIS SAMIA ANAAMINI KATIKA USHIRIKIANO NA VIONGOZI WA DINI - DKT. BITEKO

 



📌Atoa pole kwa Familia, KKKT kifo cha Askofu Sendoro

📌Kanisa Lashauriwa Kumuenzi Askofu Sendoro kwa Vitendo

📌 Waumini Waaswa Kuishi Maisha ya Kumpendeza Mungu

Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Serikali ipo tayari kushirikiana na viongozi wa dini ili kuwawezesha kutimiza majukumu yao ya kitume kwa maendeleo ya Watanzania.

Dkt. Biteko amesema hayo leo Septemba 17,  2024 katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Mwanga, Kanisa Kuu lililopo Mkoani Kilimanjaro wakati akitoa salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan mara baada ya ibada ya mazishi ya aliyekuwa Askofu wa Dayosisi hiyo, Chediel  Sendoro.

Askofu Sendoro amefariki  dunia kwa ajali ya gari iliyotokea Septemba 9, 2024  katika eneo la Kisangiro wilayani Mwanga. 

“ Rais yupo tayari kushirikiana na kanisa wakati wowote ili kanisa liweze kufanya kazi zote za kitume na sisi tuko tayari kuifanya Tanzania iwe bora na Watanzania waishi vizuri katika nchi yao,” amesema Dkt. Biteko.

Ameongeza kuwa msingi wa Dayosisi hiyo umejengwa kwa upendo na kuwa moja ya kazi kwa viongozi wa kanisa hilo ni kupata  mtu atakayeendeleza kazi na maono ya Askofu Sendoro juu ya kanisa hilo.

Amefafanua kuwa kila binaadamu ataiaga dunia itakapofika wakati wake ispokuwa kila mmoja aliyehai amefanya nini na hivyo hawana budi kukumbuka mahubiri ya Askofu Sendoro na umoja alioujenga miongoni mwao.

“ Natoa pole kwa familia, wazazi, mjane, watoto na wajukuu kwa kuwa Septemba 9, 2024 lilitokea jambo lisilo la kawaida na kuondokewa na Askofu Sendoro. Nakupa pole Askofu Mkuu wa Kanisa, maaskofu wote na Wanamwanga, tuyaenzi  yote aliyokuwa  akiyaishi, alijali sana maadili yetu naomba tena tuendelee kuliombea Taifa  na nchi yetu.” Amesisitiza Dkt. Biteko.

Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amesema kuwa Rais Samia alishatoa muongozo na uchunguzi  ufanyike haraka iwezekanavyo juu hali ya siasa na vitendo vya uvunjifu wa amani nchini. “ Nataka niwaombe kama viongozi wa kiroho muendelee kushirikiana na Serikali  kuwaombea Watanzania na kuifanya Tanzania kuwa mahali bora zaidi pakuishi.” Amemalizia  Dkt. Biteko. 

Akihubiri katika ibada hiyo Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Askofu Dkt. Alex Malasusa amesema kuwa  siku ya leo ni siku ya pekee ambayo  Askofu Sendoro amelala kwenye jeneza na kuwa ni jambo ambalo kibinadamu linatisha lakini hakuna kitakachoweza kuwatenga na tendo la Mungu.

“ Hata katika hili Mungu anaonesha pendo lake, wazazi wake na watoto wake endeleeni kuamini Mungu ameonesha pendo lake, watu wa Mwanga mlikua na Askofu endeleeni kuliangalia pendo la Mungu msiliangalie hili gumu lililotokea angalieni  pendo lake.” Amesema Askofu Malasusa.

Amesititiza “Nachotaka kukazia  hapa kile tunachosema hasa sisi wachungaji kionekane katika maisha yetu, matendo yetu na kuishi kwetu. Mtakatifu Paulo anatufundisha kuwa yuko pamoja nasi, tuangalie alama ya msalaba ni alama ya ushindi.” 

Aidha, Askofu Malasusa amewaeleza waombolezaji  kuwa walio hai wanapaswa kuishi maisha ya uhakika ili Mungu atakapowaita wawe tayari na kuwa na  ushuhuda wa kweli sio wa kusemwa na watu, na kuwa waendelee kuliombea kanisa.

Askofu Malasusa ametumia jukwaa hilo kuwataka Watanzania kushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa  baadaye  mwaka huu pamoja na Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwakani.

Aidha, amewataka viongozi wa kisiasa kukutana na kuzungumza juu ya changamoto zinazowakabili ili nchi iendelee kuwa na amani na mahali pazuri pa kuishi.

Akitoa salamu, Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee Cleopa Msuya amewataka wana Mwanga na KKKT kwa ujumla kumuenzi Askofu Sendoro kwa kuendeleza misingi imara aliyoijenga.

Amesema licha ya machungu waliyonayo waumini wanapaswa kujipanga na kupata viongozi watakaotimiza malengo yake juu ya kanisa hilo.

“ Niombe watakaotafuta mbadala wake watupatie mtu ambaye yale yote aliyoanzisha yataendelea na kutuunganisha wakristo hapa Mwanga na Dayosisi zingine. Tafuteni mtu atakaye vaa viatu vya Askofu Sendoro.” Amesema  Mzee Msuya.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Mwanga, Mhe. Joseph Tafayo amesema “ Nazungumza kwa niaba ya wananchi wa wote wa Mwanga kwa sababu yalipotokea matatizo mbalimbali Askofu Sendoro alishirikiana nasi watu wa Mwanga.”

Ameendelea kwa kusema kuwa Baba Askofu huyo aliwashirikisha waumini wa kanisa hilo katika shughuli mbalimbali wakati wa uongozi wake na kwa muenzi kwa wataendelea kushirikiana na uongozi wa Kanisa.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...