Skip to main content

SERIKALI KUONGEZA IDADI YA VIZIMBA ILI KUPUNGUZA CHANGAMOTO YA MAMBA KANDA YA ZIWA

 




 Wananchi wapongeza jitihada za Serikali.

Na Beatus Maganja 

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii na taasisi yake ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA imetenga fedha zaidi ya shilingi milioni 210 kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kwa ajili ya ujenzi wa vizimba saba Kanda ya Ziwa ili kuwalinda wananchi dhidi ya athari za wanyamapori wakali na waharibifu hususani mamba.

Kauli hiyo imetolewa Oktoba 01, 2024 na Mkuu wa wilaya ya Sengerema Mhe. Senyi Ngaga Katika ziara ya kukagua miradi ya vizimba  na kutoa elimu ya matumizi sahihi ya vizimba hivyo kwa wananchi wa Buchosa, ziara iliyofanywa na TAWA wilayani humo.

"Tunashukuru sana Kwa hii hatua ambayo imefanywa na Serikali ya kuongeza bajeti ya kujenga vizimba vingine, nimesikia bajeti hii tunayoendelea nayo imetengwa zaidi ya shilingi milioni 200 nyingine Kwa ajili ya kutengeneza vizimba zaidi ya saba " amesema Mhe. Senyi 

Mhe. Senyi pia amepongeza jitahada zinazofanywa na TAWA katika kudhibiti wanyamapori hao, kutoa elimu Kwa wananchi pamoja na mwitikio wa haraka pale wananchi wanapohitaji msaada wao.

"Tunawashukuru sana wenzetu wa TAWA kwasababu tumeona matukio yanapungua Kwa kiasi kikubwa hasa Kwenye yale maeneo ambayo tayari tumeshaweka vizimba, lakini pamoja na vizimba watu wa TAWA wanatoa elimu, kwahiyo unaona maeneo ambayo hakuna vizimba elimu inawasaidia sana" amesisitiza Mhe. Senyi.

Naye Afisa uhifadhi II kutoka Kituo kidogo cha Kanda ya Ziwa Mwanza, Mohamed Mpoto amesema katika kipindi cha miezi miwili kuanzia Julai - Septemba, 2024 jumla ya watu 1,523 kutoka vijiji vitano (Izindabo, Nyonga, Lugata, Nyachitare na Kahunda) vya Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema waliweza kufiwa na elimu ya kuepuka madhara yanaweza kusababishwa na wanyamapori wakali na waharibifu hususani mamba na viboko, elimu iliyotolewa na Maofisa wa TAWA Kwa njia ya mikutano ya hadhara.

Kwa upande wake Afisa habari wa TAWA Beatus Maganja amebainisha maeneo ambayo vizimba hivyo vitajengwa kuwa ni pamoja na vijiji vya Izindabo na Nyakasasa (Buchosa), Chinfunfu (Sengerema) na vijiji vya Kasahunga, Iramba, Butimba na Nerumba vilivyoko wilaya ya Bunda.

Ongezeko la idadi ya vizimba hivyo litaifanya Halmashauri ya Buchosa kuwa na jumla ya vizimba sita, idadi inayotajwa kuwa ni kubwa kuliko sehemu zingine zote zilizojengwa vizimba nchini.

Aidha Maganja amewasisitiza wananchi wa wilaya ya Sengerema hususani Halmashauri ya Buchosa kuwa na matumizi sahihi ya vizimba hivyo ili kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na wanyamapori hao sambamba na kuchukua tahadhari wanapokuwa wakifanya shughuli mbalimbali za kiuchumi katika ziwa Victoria.

Kufuatia hatua hiyo, wananchi wa Buchosa wameishukuru Serikali kwa jitihada na hatua mbalimbali inazozichukua Kwa ajili ya kuokoa maisha yao kwa kuwajengea vizimba ambayo wanakiri kuwa vimekuwa na msaada mkubwa kwao.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...