Skip to main content

SERIKALI YAJIPANGA KUTOKOMEZA MAGONJWA YASIYOPEWA KIPAUMBELE

 

Na Mwandishi wetu Dar 

Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imedhamiria ifikapo 2030 kutokomeza maambukizi ya magonjwa yasiyopewa kipaumbele kwenye halmashauri zote nchini humo ili kuwakinga wananchi wake na magonjwa hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri wa Afya Jenister Mhagama amesema wanatarajia hadi kufikia mwaka 2027 wawe wamevuka asilimia 95 kuelekea kutokomeza magonjwa hayo pamoja na kufanya vizuri licha ya kuwepo changamoto mbalimbali ikiwemo fedha.

Amesema kuwa katika kukabiliana na changamoto ya kupambana na magonjwa yasiyopewa kipaumbele, Serikali ya uingereza imekuwa ikiisaidia wizara ya Afya, ambapo leo wamekutana na mkamwana wa mwana mfalme wa Uingereza ili kujadili magonjwa yasiyopewa kipaumbele ikiwemo mabusha, matende na vikope (Trachoma)

"Leo tumekutana na huyu mke wa mtoto wa mfalme ili kuonyesha maeneo ambayo tumefanya vizuri, kwani Shirika la Afya duniani linataka ifikapo mwaka  2030 tuwe tumeshapambana na magonjwa haya yameondoka katika nchi zetu,”amesema Mhagama.

Amesema Serikali ya Uingereza imesaidia  katika sekta ya afya kuanzia  mwaka 1998 ambapo walitoa kiasisi cha zaidi ya Sh11.8 bilioni ambazo zimesaidia kusomesha wataalamu,tufanya upasuaji na kwenye magonjwa ya Kikope ambayo yanaweza kusababisha upofu.

Ameongeza kuwa, fedha hizo zimesaidia kununu vifaa tiba vinavyohusiana na macho  ambavyo vimepelekwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili,KCMC  na Mvumi kama kituo cha sayansi tiba.

“Yapo magonjwa mengine ambayo tumekuwa tukifanya nao kazi kama  matende, mabusha,minyoo na tumefanya kampeni ambazo zinatusaidia kuthibiti magonjwa hayo ikiwemo kufanya usafi,kunawa uso na kunawa mikono,”amesema na kuongeza .

Kwa upande wake, Meneja Mpango wa Taifa wa Kuthibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbeke ,Dk Clara Mwasusu, amesema mwaka 2012 Serikali ilianza kutokomeza ugonjwa wa Kikope kwenye halmashauri 69 ambapo  wananchi wanaoishi kwenye maeneo ambayo hatarishi wamekuwa wakiwezeshwa dawa.

Dk Mwasusu amesema mwaka huu wameweza kutokomeza ugonjwa huo kwenye halmashauri 60 kati ya hizo tisa bado wanaugua ambapo matarajio yao ifikapo mwaka 2017 wanatarajia kutokomeza ugonjwa huo.

“Watu 167 waliathirika na ugonjwa wa Kikope na tuliwafanyia upasuaji  ili kuwakinga na upofu wa kudumu na hivi sasa tumebakiwa na wananchi zaidi ya 10 milioni ambao wapo kwenye halmashauri 20  kati ya hizo 16 wanaendelea kupatiwa huduma,”amesema

Amezungumzia ugonjwa wa Kichocho bado ni tatizo kwa sababu hawajaweza kuudhibiti kwa vile ipasavyo wanatarajia Serikali na mahusiano mazuri ya nchi ya Uingereza watafikia malengo ya kutokomeza ugonjwa huo.

Dk Mwasusu amesema wanatarajia kuanza  utekelezaji wa huduma ya bima kwa wote wananchi wa hali ya chini wataweza kupata hiozo huduma kwa kuwa gharama yake ni kubwa wanatakiwa kulipia kuanzia Sh250,000 hadi Sh 300,000



Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...