Skip to main content

DKT.BITEKO ATAKA UMOJA, USHIRIKIANO NA UBUNIFU TAASISI ZA NISHATI



📌 *Asema Rais Samia anataka Ubunifu ili kusogeza huduma bora kwa wananchi*

📌 *Asisitiza utendaji kazi umuangalie Mtanzania wa kawaida anayeitegemea Serikali kubadili maisha*

📌 *Aagiza kila Taasisi kuwa na Vigezo vya Upimaji Utendaji Kazi*

📌 *Ataka Watendaji waache alama ya kazi, si kulinda vyeo*



Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka Watendaji na Watumishi katika Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati kuwa na umoja, ushirikiano na ubunifu ili kusogeza huduma bora kwa wananchi  ikiwemo za umeme, mafuta,na Nishati Safi ya Kupikia.

Amesema hayo tarehe 28 Oktoba, 2024 jijini Dodoma wakati wa Kikao chake na Menejimenti ya Wizara ya Nishati na Taasisi zilizo chini yake ambacho ni cha pili kutoka uanzishwe mfumo  mpya ndani ya Wizara na Taasisi zake wa kujifanyia tathmini ili kuona namna inavyofanya kazi ya kuhudumia wananchi.

“Ikumbukwe kuwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wote amekuwa akisisitiza kuwepo na ubunifu kwenye Wizara na Taasisi ili kusogeza huduma za uhakika  kwa wananchi na huduma hizo bora haziwezi kutokea  kama hakuna umoja na ushirikiano ndani ya Taasisi za Serikali.” Amesema Dkt. Biteko



Katika Kikao hicho, Dkt. Biteko amewataka watendaji wa Wizara na Taasisi kufanya kazi kwa bidii na weledi huku wakimuangalia mtanzania wa kawaida anayetegemea mipango ya Serikali ili kuweza kubadili maisha yake  na kukumbuka kuwa Sekta ya Nishati ni injini ya uchumi wa nchi hivyo inapotetereka yanatokea  matatizo kwenye nyanja zote za kiuchumi na hali ya maisha ya watu.

Vilevile amewakumbusha watendaji wa Wizara na Taasisi kutochukua muda mwingi kulinda vyeo bali kinachotakiwa ni matokeo ya  kazi  zitakazoacha alama kwenye Taasisi kwani vyeo huwa havidumu.

Pamoja na kupongeza Wizara ya Nishati na Taasisi zake kwa kuwa na  mchango katika ukuaji wa uchumi wa nchi, ametaka kila Taasisi kuwa na Vigezo vya Upimaji wa Utendaji Kazi vitakavyotumika kufanya tathmini ya  uelekeo wa Sekta ya Nishati nchini.

Dkt. Biteko amewasisitiza Watumishi wote kutenda  zaidi kuliko kusema, kujenga taasisi imara kuliko mtu imara na  kujenga Sekta ya Nishati imara kuliko Waziri imara ili kuweza kuwahudumia wananchi vizuri na kwa haraka.



Aidha, ameagiza Watendaji kueleza mafanikio ya Sekta ya Nishati kwa watanzania ili wafahamu jinsi Rais Samia anavyojitoa katika kuiendeleza Sekta ya Nishati.

Vilevile, Dkt. Biteko ameagiza kufanyike tathmini ya Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwa lengo la kufahamu mwelekeo wa utekelezaji wa mkakati huo na kuendelea kuboresha utekelezaji wake.

Katika kikao hicho cha Menejimenti ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake pia ilitolewa tathmini ya utendaji kazi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara iliyofanyika katika kipindi cha miezi mitatu kinachoishia mwezi Septemba 2024 ambapo  Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeongoza kwa kufanya vizuri ukifuatiwa na Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA).



Aidha, kwa tathmini ya utendaji kazi iliyofanyika ndani ya TANESCO, mikoa ya Kitanesco ya Singida, Kinondoni Kaskazini na Manyara imefanya vizuri zaidi katika kutoa huduma bora kwa wananchi.

Washindi wa tathmini hiyo ya utendaji kazi wamepatiwa zawadi ikiwemo barua za pongezi huku wale ambao hawakuvuka kiwango cha asilimia 80 wakitakiwa kuongeza juhudi.

Awali, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba alisema kikao hicho ni mahsusi kwa ajili ya kufanya tathmini ya utendaji sekta ya Nishati kwa Wizara na Taasisi zake.



Taasisi zilizoshiriki kikao hicho ni Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika la Maendeleo ya Petroli  Tanzania (TPDC), Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA), Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi Tanzania (TGDC).





Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...