Skip to main content

KONGAMANO LA JOTOARDHI AFRIKA KULETA UWEKEZAJI NA UBUNIFU MPYA TANZANIA -MHE. KADUARA



📌 *Asema ARGeo-C10 itasaidia  Afrika kufikia suluhisho la upatikanaji Nishati Safi*

📌 *Awaita Washirika wa Maendeleo kuendeleza Jotoardhi Tanzania*

📌 *Dkt.Mataragio asema Tanzania imetumia ARGeo-C10 kutangaza hazina ya Jotoardhi*

📌 *Shirikisho la Jotoardhi Afrika (AGA) lasema ni Kongamano la aina yake*



Waziri wa Maji, Nishati na Madini wa Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar, Mhe. Shaibu Kaduara amesema Kongamano la Kimataifa la Jotoardhi Afrika (ARGeo-C10) lililofanyika nchini kuanzia tarehe 21 Oktoba 2024 litaleta uwekezaji na ubunifu mpya katika uendelezaji wa nishati ya Jotoardhi Tanzania.

Mhe. Kaduara amesema hayo wakati hafla ya ufungaji wa kongamano hilo iliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 25 Oktoba, 2024.

“Maarifa na utaalam uliopatikana katika kongamano hili utasaidia mustakabali wa Tanzania na Afrika katika kufikia suluhisho la upatikanaji wa nishati safi, kuongeza kasi ya maendeleo ya  jotoardhi Tanzania na kuongeza mchango wa nishati jadidifu katika uzalishaji umeme.” Amesema Kaduara



Amesema Tanzania imepata heshima kubwa baada ya kuandaa  kongamano hilo kwa mafanikio na imekuwa ni fursa ya  kutangaza maeneo yake yanayohitaji uendelezaji ikiwemo eneo la Ngozi mkoani Mbeya ambapo kunachimbwa visima vitatu vya uhakiki wa mashapo ya Jotoardhi.

Ameongeza kuwa, kwa kuandaa kongamano la ARGeo-C10 Tanzania imeonesha kwa vitendo nia yake ya kuendeleza jotoardhi, kushiriki katika biashara ya hewa ukaa na kutokuwa na uzalishaji wa hewa ya ukaa.

Mhe. Kaduara ametumia fursa ya kongamano hilo kuwasihi Washirika wa Maendeleo duniani kuendelea kuunga mkono jitihada za kukuza nishati ya Jotoardhi barani Afrika.



Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio,  amesema Kongamano la ARGeo-C10 limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani Nchi 14 ambazo ni Wanachama wa Shirikisho la Jotoardhi Afrika zimeshiriki pamoja na nchi nyinginezo zipatazo 12.

Ameongeza kuwa Kongamano pia limehusisha Wataalam wabobezi kutoka mataifa hayo 26 ambao wametoa mafunzo maalum katika Jotoardhi ikiwemo masuala ya tathmini ya Jotoardhi na jinsi nishati hiyo itakavyosaidia kuangalia masoko ya hewa ya ukaa.

Amesema kupitia Kongamano hilo nchi nyingi zimeonesha nia ya kuwekeza Tanzania baada ya kuona utajiri wa jotoardhi uliopo na utayari wake katika kushirikiana na nchi nyingine duniani ili kuiendeleza.

Amesema nchi nyingi Afrika bado hazijatumia nishati hiyo ipasavyo hivyo Kongamano la ARGeo-C10 limelenga kuharakisha uendelezaji nishati ya Jotoardhi Afrika ili iwe na mchango mkubwa katika gridi za umeme kama ilivyo kwa vyanzo vingine kama vile maji.



Mwakilishi wa Spika la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Joseph Mhagama amesema kongamano hilo la Jotoardhi limewawezesha Wabunge walioshiriki kupata uelewa kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo matumizi ya moja kwa moja ya Jotoardhi, fursa, changamoto na biashara ya hewa ukaa hivyo uelewa huo utawasaidia kutoa ushauri kwa Serikali na kuisimamia Sekta ya Jotoardhi kwa ujumla.

Naye, Mkuu wa Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Mazingira Duniani (UNEP) katika nchi za Kusini mwa Afrika, Meseret Teklemarian ameshukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendesha kongamano la ARGeo-10 kwa mafanikio makubwa  huku likipewa msukumo mkubwa na Serikali na kwamba UNEP itaendelea kuunga mkono Tanzania kwa namna mbalimbali ili kuendeleza nishati ya Jotoardhi.

Dkt. Peter Omenda, Rais wa Shirikisho la Jotoardhi Afrika (AGA), naye ameishukuru Tanzania kwa kuendesha kongamano hilo kwa mafaniko na kueleza kuwa ni kongamano bora linalopaswa kuigwa na nchi nyingine Afrika.



Ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kujitoa ipasavyo katika kuhakikisha kuwa Kongamano hilo linafanikiwa huku likiwa na washiriki wengi zaidi kuliko makongamano mengine yaliyopita.

Aidha ameeleza kuwa,  Kongamano linalofuata litafanyika Comoro mwaka 2026.

Awali, Meneja Mkuu wa Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC), Mathew Mwangomba alisema ARGeo-C10 imeacha alama na kumbukumbu barani Afrika ambapo ameishukuru Serikali na wadau kwa kuwezesha kongamano hilo kufanyika kwa mafanikio.

Amesema Tanzania ipo tayari kushirikiana na wadau wengine ili kuendelea Jotoardhi kupitia utaalam na uwekezaji kwenye maeneo yenye mashapo ya Jotoard.



Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...