Skip to main content

TUNAIMARISHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA MIUNDOMBINU YA NISHATI ILI KUFIKISHA HUDUMA KWA WOTE- DKT.MATARAGIO



📌 *Asisitiza nia ya Serikali ni kutoa huduma stahiki bila kuangalia umbali au kipato*

📌 *Apongeza kampuni ya Puma Energy Tanzania kushirikiana na Serikali uhamasishaji Nishati Safi ya Kupikia*

📌 *Puma Energy Tanzania yaahidi kuendeleza ushirikiano*

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati,  Dkt. James Mataragio amesema Serikali inaendelea kuimarisha mazingira ya uwekezaji  na miundombinu ya Sekta ya Nishati nchini ili  kuwezesha wananchi kufikiwa na huduma stahiki bila kujali umbali na vipato vyao.

Dkt. Mataragio ameyaeleza hayo  jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya utoaji Tuzo kwa Mawakala na Wadau wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania ambayo  inaunga mkono juhudi za Serikali za kuelimisha jamii kuhusu matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kupitia bidhaa za Puma Gas.

Dkt. Mataragio amesema  moja ya majukumu ya Wizara ya Nishati ni kukutana na wadau mbalimbali wakiwemo watoa huduma na watumiaji ili kuimarisha ushirikiano kati ya  sekta binafsi na Serikali utakaopelekea utoaji wa huduma bora kwa wananchi  ikiwa ni moja ya vipaumbele vya Serikali.

Katika hafla hiyo,  Dkt.Mataragio ameipongeza  kampuni ya Puma  kwa jitihada  zinazounga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuhamasisha jamii ili itumie Nishati Safi ya Kupikia na hivyo kutimiza lengo la asilimia 80 ya Watanzania kutumia Nishati Safi ya Kupikia ifikapo mwaka 2034.

Amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa Balozi na kinara katika kuhamasisha matumizi ya Nshati Safi ya Kupikia nchini na Duniani ili  kuhakikisha Watu wanaondokana na matumizi ya kuni na mkaa ambao una madhara kwa  afya na kusababisha uharibifu wa mazingira.

Kuhusu Tuzo hizo zilizotolewa na Puma Energy Tanzania  kwa Mawakala na Wadau mbalimbali nchini, Dkt.Mataragio ameelekeza kuwa  ziwe chachu ya kuendelea kufanya kazi kwa weledi na ufanisi kulingana na vigezo na mashariti ya Kampuni kwa maslahi ya jamii. 

Amesema kupitia mfano uliooneshwa na Puma Energy Tanzania wa kuwakutanisha wadau wake kila mwaka ili kuzungumzia mafanikio na changamoto zilizopatikana, iwe ni chachu kwa  kampuni nyingine kuiga mfano huo ambao unasaidia kukuza sekta ya Nishati nchini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Bi. Fatuma Abdallah ameishukuru Serikali kwa hatua mbalimbali za kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia na kuahidi kuendelea kuunga mkono juhudi hizo kwa kuwafikishia wananchi bidhaa ya Puma Gas kupitia kwa Mawakala na Wadau waliopo maeneo mbalimbali.

Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Kamishna wa Petroli na Gesi, Godluck Shirima.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...