Skip to main content

VIONGOZI WA DINI WATAKIWA KUTOA ELIMU YA MAGONJWA YA MLIPUKO



Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel ametoa rai kwa Viongozi wa Dini kote nchini, kutumia majukwaa yao kusaidia Serikali kutoa elimu sahihi ya kuepuka na kukabiliana na magonjwa ya mlipuko kama Mpox, Kipindupindu na Marbug.

Dkt. Mollel ameyasema hayo jijini Dar es Salaam  wakati akimuwakilisha Waziri wa Afya  Jenista Mhagama kwenye Mkutano wa Waziri wa Afya na viongozi wa Dini kuhusu tahadhari dhidi ya magonjwa ya mlipuko na suala la Bima ya Afya kwa Wote.



Amesema viongozi hao wana wajibu wa kiroho wa kusaidia kuhakikisha wanailinda jamii na maradhi yanayoepukika kwa kutumia majukwaa yao ya ibada.

"Tunazungumza nanyi kwa niaba ya waumini, viongozi wa dini kote nchini isaidieni Serikali kutoa elimu sahihi ya kuepukana na magonjwa ya mlipuko kama Mpox, Kipindupindu na Marbug,"amesema Dkt. Mollel.



Ameongeza kuwa jitihada za Serikali ya awamu ya Sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendeleza jitihada za afua mtambuka ili kuhakikisha nchi inabaki salama.

"Wakati tukifuatilia wasilisho tumeona ramani ya Tanzania ikiwa nyeupe lakini wenzetu wanao tuzunguka wameshapata visa vya baadhi ya magonjwa ya mlipuko, sasa niwaombe muemde mkazungumze na wanajamii ili ramani ya Tanzania izidi kubaki nyeupe,” amefafanua Dkt. Mollel



Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. John Jingu akihitimisha mkutano huo amesema ipo haja ya pande hizo mbili kuendelea kufanya kazi kwa pamoja ili  wananchi ambao niwaumini kwenye nyumba za ibada  kuwa salama na kuendelea na majukumu yao.

"Tumekubaliana tunatoka hapa tukiwa na nia moja, tunaenda kuwahimiza waumini wetu lakini pia na sisi wenyewe kwa usafi ndio kila kitu, baadhi ya mila na desturi zetu zinazokuwa hatarishi tuziepuke na sisi tuwajibike na kuhakikisha tunaendelea kuwa salama na mwisho wa siku nchi yetu kwa ujumla itakuwa salama,"amesema Dkt. Jingu.



Kwa upande wao wawakilishi wa viongozi wa dini  wameipongeza Serikali kwa kutumia majukwaa ya dini kuendelea kufikisha elimu ya afya kwa umma na kuahidi kwenda kuwahimiza waumini dhidi ya magonjwa hatarishi ya mlipuko

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...