Skip to main content

MAKUYUNI WILDLIFE PARK KUFUNGUA NJIA YA MAFANIKIO YA WATALII









Bodi ya TAWA yaridhishwa na uboreshaji wa miundombinu ya utalii

Na Beatus Maganja, Arusha.

 MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imeanza rasmi utekelezaji wa mikakati ya kuiendeleza na kuiandaa  Hifadhi ya Makuyuni Wildlife Park iliyopo Mkoani Arusha Kwa ajili ya kupokea wageni wengi zaidi kwa kuongeza mindombinu ya utalii hususani barabara, ujenzi wa mabwawa ya maji Kwa ajili ya wanyamapori na kuondoa mimea vamizi ndani ya eneo hilo.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TAWA Dkt. Simon Mduma katika ziara ya wajumbe wa Bodi hiyo ya kukagua ujenzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na TAWA ndani ya Hifadhi ya Makuyuni Wildlife Park.

"Hifadhi hii ni mpya ilikabidhiwa takribani mwaka mmoja uliopita na katika mchakato wakuiendeleza na kuiandaa Kwa ajili ya kupokea wageni kulikuwa na umuhimu wa kuongeza barabara kwenye maeneo haya ili wageni watakaokuwa wanatembelea eneo hili wawe na wigo mpana wa kuiona mandhari nzuri sana ya eneo hili lakini vilevile kutoa nafasi kubwa ya kuona vivutio ambavyo vipo kwenye hifadhi hii" amesema Dkt. Mduma

"leo tumezunguka na tumeona maendeleo ya ujenzi wa barabara, ni kazi ambayo inaridhisha, ni nzuri na ratiba ambayo ipo kwa makubaliano kwenye  mikataba Kazi ya ujenzi wa barabara inaendelea vizuri sana hilo tumeridhika nalo" ameongeza" Mduma.

Dkt. Mduma amesema kutokana na eneo la Makuyuni kukumbwa na changamoto ya ukame wakati wa kiangazi kiasi cha kusababisha wanyamapori kutoka nje ya hifadhi hiyo na kwenda kwenye makazi.ya watu, Bodi ya TAWA iliona umuhimu wa kujenga bwawa la kukusanyia maji Kwa ajili ya wanyamapori, hivyo Bodi hiyo imefanya ukaguzi wa eneo litakapochimbwa bwawa hilo na kuridhishwa nalo, na hivyo ujenzi wake utaanza hivi karibuni kwakuwa mikataba imekwisha sainiwa tayari Kwa kuanza kazi hiyo.

Kwa upande wake mjumbe wa Bodi hiyo Profesa Suzanne Augustino ameipongeza Menejimenti ya TAWA na watumishi wote Kwa jitihada kubwa wanayoifanya kuboresha mazingira ya Makuyuni Wildlife Park ikiwa ni pamoja na kufanyia kazi ushauri na maelekezo yanayotolewa na Bodi hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake Mej. Jen. (Mstaafu) Hamis R. Semfuko.

Aidha Profesa Suzanne ametanabaisha kuwa kutokana na kuendana na kasi ya Rais wa awamu ya Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa Balozi wa utalii wa nchi yetu na uwekezaji wa miundombinu ya utalii unaofanywa na TAWA, Makuyuni Wildlife Park ya miaka mitano ijayo  haitakuwa kama inayoonekana leo badala yake itakuwa Makuyuni yenye mabadiliko makubwa ambayo inafungua njia kwa watalii wengi zaidi lakini pia Makuyuni yenye utofauti mkubwa na maeneo mengine yenye vivutio vya utalii.

Naye Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi ambaye pia ni Kaimu Kamanda wa Uhifadhi Kanda ya Kaskazini ya TAWA Privatus Kasisi amesema Kitendo cha Serikali kuiamini TAWA na kuikabidhi eneo hilo muhimu  kumeipa chachu na nguvu ya kuliendeleza na kulisimamia kwa ukamilifu ili kulifanya liwe bora kwa manufaa ya wakazi wa Mkoa wa Arusha na Taifa Kwa ujumla.

Aidha Kasisi amesisitiza kuwa TAWA itahakikisha inaongeza kasi ya uboreshaji wa miundombinu ya eneo hilo ili kupata watalii wengi na mapato kwa muda mfupi hasa katika mashindano ya AFCON ya mwaka 2027 ambapo Tanzania inatarajia kupokea wageni wengi kutoka mataifa mbalimbali na Arusha ni moja ya miji ambayo itapokea wageni hao.

Katika hatua nyingine, Kamanda wa eneo la Makuyuni Wildlife Park Andrew Kishe amesema miradi yote inayotekelezwa na TAWA ndani ya Hifadhi hiyo inagharimu zaidi TZS Billioni moja ambayo inajumuisha barabara atakazopewa mkandarasi na zile zinazotengenezwa Kwa kutumia vitendea kazi vya taasisi huku akibainisha kuwa barabara zinazofunguliwa zina mrefu wa Kilometa 18.

Vilevile miradi hiyo inajumuisha ujenzi wa geti kubwa la kisasa la watalii na  bwawa la maji Kwa ajili ya wanyamapori ambapo ujenzi wa miradi yote hiyo inatokana na fedha za ndani ya taasisi ya TAWA.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...