Skip to main content

WAZIRI MAVUNDE AWAKARIBISHA WAWEKEZAJI WA MADINI KUTOKA FINLAND KUWEKEZA NCHINI TANZANIA







▪️Ampongeza Rais Samia kwa kuboresha mazingira ya Biashara nchini

▪️Wavutiwa na uwepo wa Rasilimali madini za kutosha

▪️Finland yaiahidi Tanzania ushirikiano kwenye utafiti wa madini

Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde amewakaribisha jumuiya ya wa Wafanyabiashara kutoka Nchini Finland kuwekeza kwenye sekta ya madini kwa kuwa nchi ya Tanzania imejaaliwa kuwa na rasilimali ya kutosha ya madini,mazingira ya uwekezaji rafiki na sera zinazotabirika.

Waziri Mavunde ameyasema hayo jana  Masaki Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa kifungua kinywa ulioandaliwa na Ubalozi wa Finland nchini kwa lengo la kuwakutanisha wafanyabiashara wa Madini kutoka Finland na Wizara ya Madini ili kubaini maeneo ya ushirikiano na fursa za kiuchumi zilizopo sekta ya madini nchini Tanzania.

Akizungumza katika hafla hiyo Balozi wa Finland nchini Tanzania Mh. Theresa Zitting amesema Tanzania na Finland ni nchi zenye ushirikiano mkubwa kwenye masuala ya kiuchumi na hivyo ni wakatinmuafaka sasa kuimarisha mahusiano hayo kupitia uwekezaji kwenye sekta ya madini ambapo amepongeza hatua kubwa zinazofanywa na Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kukuza sekta ya madini nchini na kuifanya kuwa sekta muhimu kwenye kuchangia maendeleo ya uchumi ya Tanzania.

Naye Mkurugenzi  Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti Madini ya Finland (*GTK*) Prof. Tiilikainen Kimmo amesema kwamba kupitia makubaliano (*MoU*) kati ya GTK na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini(*GST*),Finland itashirikiana na Serikali ya Tanzania kuimarisha shughuli za Utafiti wa madini ili kuiwezesha Tanzania kufikia Dira ya 2030 ya Madini ni 𝐌𝐀𝐈𝐒𝐇𝐀 𝐧𝐚 𝐔𝐓𝐀𝐉𝐈𝐑𝐈 ambapo Tanzania imejipanga kufanya utafiti wa kina wa madini wa kufikia eneo la 50% la eneo la nchi nzima.

Akiwasilisha hotuba yake Waziri wa Madini *Mh. Anthony Mavunde* amewakaribisha wafanyabiashara kutoka Finland kuja kuwekeza nchini Tanzania kwa kuwa Tanzania ina fursa nyingi za kiuchumi kupitia sekta ya madini na hasa madini mkakati ambayo kwa sasa yana uhitaji mkubwa Duniani.

“Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kupitia Falsafa yake ya uongozi wa 4R ameweka mazingira rafiki ya biashara na uwezekaji nchini Tanzania na hivyo Tanzania ni sehemu salama ya kufanya uwekezaji.

Tanzania imejaaliwa rasilimali madini ya kutosha na hivyo kuifanya nchi yetu kuwa na nafasi nzuri kuvutia uwekezaji.

Hivyo tunafungua milango kwa wafanyabiashara kutoka nchini Finland kuchangamkia fursa za uwekezaji kupitia sekta ya madini“Alisema Mavunde

Wafanyabiashara hao wapo nchini kuhudhuria mkutano wa Kimataifa wa Madini na Uwekezaji 2024 unaofanyika nchini Tanzania.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...