Skip to main content

AZAM MEDIA YAWAPA WATEJA WAKE OFA HII, YAZINDUA TAMTHILIA 3 KWA MPIGO



Na Mwandishi wetu, Dar 

KAMPUNI ya Azam Media Ltd kupitia msimu huu wa sikukuu ya Christmas imezindua tamthilia tatu kwa mpigo ambazo zinakwenda kutoa elimu kwa watazamaji wake sambamba na kuwapatia  burudani isiyo kifani na kukonga nyoyo zao.

Akizungumza Jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa tamthilia hizo Msimamizi Mkuu wa chaneli ya  Sinema Zetu, Sophia Mgaza amezitaja tamthilia hizo kuwa ni Kombolea, Tufani pamoja na Kiki ambazo zimeandaliwa kwa ubunifu mkubwa.



"Tamthilia ya Tufani itaanza kuonyeshwa Desemba 9,2024 kuanzia Jumatatu hadi Alhamisi saa 1:30 usiku,Kombolela itaanza kuonyeshwa Disemba13,2024 siku ya ,ijumaa hadi jumapili saa 1:00 usiku,huku tamthilia ya Kiki itaanza kuonyeshwa Desemba 16 ,2024 jumatatu hadi Alhamisi saa 1:00 usiku,ambapo tamthilia zote hizi zitaonekana kupitia chaneli namba 106 Sinema zetu HD" amesema Mgaza
Nakuongeza kuwa" Lengo la Azam Media Ltd kuendelea kutoa burudani ya hali ya juu kwa watazamaji Wetu huku tukisukuma Sanaa yetu kimataifa hasa katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara na popote.

Aidha amesema kuwa  Azam TV Max inawakaribisha watazamaji  kuungana nao msimu huu wa sikukuu huku wakiendelea kufurahi ofa ya kisimbuzi cha Antenna bure kwa kulipia kifurushi cha miezi miwili cha shilingi elfu ishirini na nane( 28000/= ) tu.
Aidha Mgaza amefafanua kuwa tamthilia hizo tatu ambazo ni Kombolela,Tufani na Kiki  zimewahusisha wakongwe wa uzalishaji wa filamu na tamthilia nchini pamoja na waigizaji nguli ,maarufu na wabobevu katika Sanaa ikiwa ni kutoa burudani ya aina yake kupitia Sanaa hiyo.

Akizungumza kando ya uzinduzi huo Jacob Steven maarufu JB, amesema kuwa kwasasa soko la tasnia ya filamu na tamthilia linazidi kukua huku akiipongeza Azam Media Ltd kwa kuleta Mapinduzi makubwa kwenye tasnia hiyo ambayo imechangia kuleta ajira kwa Vijana wenye vipaji vya uigizaji.

Tamthilia ya Tufani imeandaliwa na Kampuni ya JB Film Company, huku tamthilia ya Kombolela imeandaliwa na Nabra Creative Company,ambapo Tamthilia ya Kiki imeandaliwa na Magazijuto Pictures.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...