Skip to main content

GAVU AJIVUNIA UTEKELEZAJI WA ILANI JIMBO LA CHWAKA,AMPONGEZA RAIS MWINYI



*Akabidhi vifaa mbalimbali vyenye thamani ya mamilioni ya fedha katika Jimbo la Chwaka

MWAKILISHI wa Jimbo la Chwaka visiwani Zanzibar ambaye pia ni Katibu wa Halmashauri Kuu((NEC) Oganaizesheni Issa Gavu amesema Serikali ya Awamu ya Nane chini ya Rais Dk.Hussein Ali Mwinyi imefanya maendeleo makubwa kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu.



Sambamba na hayo amesema wananchi wa Jimbo la Chwaka wameendelea kushuhudia changamoto mbalimbali zikipatiwa ufumbuzi pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya barabara,elimu,afya na maji huku akielezea wazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndicho kilichokuwa na uthubutu na utayari wa kuwatumikia wananchi.

Gavu ameyasema hayo leo Desemba 14,2024 alipokuwa akielezea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu katika Jimbo la Chwaka ambapo pia amekabidhi pikipiki 20 zenye thamani ya Sh.milioni 72 , Vifaa vya michezo vyenye thamani ya Sh.milioni 17.



Pia amekabidhi  vitenge ,fulana na kofia vyenye thamani ya Sh.milioni  14 , michango kwa jamii milioni 22,vyarahani 100 thamani ya Sh.milioni 30,bati,saruji na vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya Sh.milioni Saba pamoja na mashine 15 za kuprintia ambapo kila Moja thamani ni zaidi ya Sh.milioni 2.1.

Akieleza zaidi amesema hana shaka katika uchaguzi ujao viongozi kuanzia diwani, Mbunge na Mwakilishi pamoja na Rais watatoka Chama Cha Mapinduzi huku akifafanua kuna vyama 19 lakini hakuna chama, jumuiya wala taasisi yenye utayari na uthubutu wa kuweza kuliongoza Taifa letu kwa mfanisi na mafanikio makubwa kama wanayoyaona kwa Chama Cha Mapinduzi.



"Sisi watu wa Chwaka ni mashahidi na ni mashuhuda kwenye serikali hii ya Awamu ya nane yako mambo yalikuwa yanatukwaza , Serikali hii ya CCM chini ya uongozi wa Dk.Hussein Ali Mwinyi tumepiga hatua kubwa sana katika maendeleo ndani ya watu wa Jimbo la Chwaka.

"Yapo maeneo tulikuwa na changamoto za maji , elimu ,afya sambamba na miundombinu lakini leo hii jitihada na mipango ya Serikali kila mmoja wetu anaiona kama haijakamilika basi iko kwenye mchakato,kama haiko katika mchakato iko katika mfumo wa kutafuta utaratibu mzuri wa kufanikisha kuondoa changamoto hizo.



"Tunayo miradi ya kitega uchumi kwa ajili ya kuwezesha wajasiriamali, tunavyo vyuo vya ufundi pamoja na vituo vya elimu,hayo yote ni matunda ya kukichagua  Chama Cha Mapinduzi.Ninachokuombeni watakapokuja wenzetu kuja kuzungumza nanyi msiwakasirikie wala msigombane nao.

"Sisi hoja yetu tutakwenda kuijibu kwa vitendo lakini  tunawajibu wa kujiandaa vizuri na utakapofika wakati wa kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura Jimbo letu liwe na malengo ya kufikia ufanisi kwa asilimia 100 katika uboreshaji wa daftari la kupiga kura,"ameelezea Gavu.



Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...