Skip to main content

KAWAIDA ATOA UJUMBE MZITO KWA VIJANA KUUANZA MWAKA 2025

Na Mohamed Ali Kawaida, _Mwenyekiti wa UVCCM Taifa_

Ndugu vijana wenzangu!

Tukiwa tunaanza safari ya mwaka mpya wa 2025, nipende kutumia  fursa hii kuwatakia heri ya mwaka mpya, afya njema, na mafanikio tele. Mwaka mpya ni fursa mpya. Ni ukurasa mwingine wa kitabu cha maisha yetu, kitabu ambacho tunaendelea kukiandika sisi wenyewe kwa bidii na maarifa yetu.

Tunapokabiliana na changamoto mbalimbali, ni muhimu tukumbuke kwamba ushindi wetu haupo katika kushindana na wengine, bali katika juhudi zetu binafsi huku tukiwatakia mema wenzetu. Pia umoja na mshikamano wetu kama vijana ndiyo silaha yetu kubwa ya mafanikio.

Katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wangu kama Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), nimeona kwa macho yangu nguvu, uthubutu, na bidii za vijana wa Kitanzania katika kulijenga taifa letu. Japokuwa changamoto zipo, lakini fursa ni nyingi mbele yetu, fursa ambazo tukiweza kuzitumia vizuri  zitabadilisha maisha yetu na kuleta faida katika taifa letu. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutufikisha hapa tulipo. Nawashukuru pia viongozi wenzangu wa UVCCM kutoka katika ngazi zote taifa hadi matawi na kila mwanachama ambaye amechangia mafanikio yetu.

_Vijana wenzangu, taifa letu linahitaji nguvu zetu, mawazo yetu, na maono yetu_. Kama alivyowahi kusema Nelson Mandela, *“It always seems impossible until it’s done.”* Tusikate tamaa. _Tusirudi nyuma. Kila hatua tunayochukua inachangia kujenga Tanzania yenye haki, maendeleo, na usawa_.

John F. Kennedy aliwahi kusema,

"Ask not what your country can do for you, ask what you can do for your country."

Kauli hii inatufundisha kwamba jukumu letu kama vijana ni zaidi ya kusubiri, bali ni tuna paswa kuchukua hatua leo ili kuleta mabadiliko chanya leo na kesho.

Tunapojipanga kwa mwaka huu mpya wa 2025, ni lazima tuendelee kujitoa kwa bidii katika kazi, elimu, biashara, kilimo, siasa, na shughuli nyingine za uzalishaji. _Kila hatua tunayopiga leo ni msingi wa taifa lenye ustawi, umoja, na heshima kwa vizazi vya leo na  kesho_.

Mwaka 2025 ni mwaka wa ushindi kwa vijana wa Kitanzania pia tukumbuke ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani niwaombe tuzidi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la Mpiga Kura na tuendelee kuiombea nchi yetu amani na utulivu, tukiombee Chama chetu Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan

_Nawatakia mwaka mpya wenye baraka, maendeleo, na mafanikio makubwa._ Mungu ibariki Tanzania, Mungu wabariki Vijana wenzangu.

Ahsanteni Sana.

Wenu

Mohamed Ali Kawaida

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...