Skip to main content

ZOEZI LA KULIPA FIDIA WANANCHI NGOMBO LINAKWENDA VIZURI : DC MALINYI









 Waliohama kupokelewa vijiji jirani, waipongeza Serikali 

Na Beatus Maganja, Malinyi.

Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe. Sebastian Waryuba amesema zoezi la kuwalipa fidia wananchi wa Kijiji cha Ngombo kilichopo ndani ya Pori la Akiba Kilombero Mkoani Morogoro linaendelea vizuri ambapo asilimia 93 ya wananchi wote tayari wamekwishalipwa fidia zao kwa ajili ya kupisha shughuli za uhifadhi katika Hifadhi hiyo na asilimia 7 ya wananchi waliosalia wanaendelea kushughulikiwa ili kukamilisha malipo yao.

Akizungumzia zoezi hilo Desemba 31, 2024 wilayani humo Mhe. Sebastian amesema Serikali imetoa zaidi ya shilingi billioni 6.9 kulipa wananchi 1,056  ili waweze kuhama kwa hiari kutoka maeneo ya Hifadhi huku akitoa maelekezo kwa watendaji wa vijiji 32 wilayani Malinyi kuwapokea ili waweze kuendelea na shughuli zao za kila siku.

"Kwanza si kweli kwamba wananchi wa Ngombo hatujawaambia mahali pakwenda. Katika barua yangu ya tarehe 4 Disemba, 2024  niliyowaandikia watendaji wa vijiji 32 vilivyo ndani ya wilaya ya Malinyi, nilitoa maelekezo ya kuwapokea wananchi wa Kijiji cha Ngombo wanaopisha shughuli za uhifadhi katika Pori la Akiba Kilombero, na ndivyo inavyofanyika na pia nilielekeza watendaji hao wawataarifu wananchi wote kupitia mikutano ya hadhara" amesema

"Na tangu wananchi wangu wa Ngombo walipoanza kuhama kwenda katika maeneo yao waliyokwenda, sijapata lalamiko lolote kwa simu au kwa mdomo kwamba wamezuiliwa kukaa mahali fulani na kwa taarifa nilizonazo baadhi yao wamehamia sehemu mbalimbali ikiwemo Mikoa ya Lindi, Ruvuma, Pwani na Halmashauri ya Mlimba. Kwahiyo mimi ninaamini mambo yanakwenda vizuri na ndivyo ilivyo" amesisitiza Mhe. Sebastian.

Kuhusu wanafunzi waliokuwa wanasoma shule katika Kijiji cha Ngombo, Mkuu huyo wa wilaya amesema amekwishatoa maelekezo  kwa Afisa elimu kuwapokea na kuwasajili  katika shule zilizopo kwenye vijiji vilivyo ndani ya wilaya hiyo bila masharti yoyote ili waweze kusoma kwa uhuru.

Aidha, Mhe. Sebastian amesema wananchi wa Kijiji cha Ngombo waliandaliwa mapema kwa kupewa elimu juu ya malipo ya fidia ili weweze kuhama kutoka katika eneo la Hifadhi ya Kilombero tangu mwezi Agosti, 2024. Hivyo, walikuwa na uelewa kuhusu zoezi hilo na amewataka kuepuka watu wenye nia ovu ya kupotosha dhamira njema ya zoezi hilo.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kata ya Biro Bi. Elizabeth Mnenuka amekiri kupokea zaidi ya wananchi 50 katika Kijiji cha Biro na wengine zaidi ya 30 katika Kijiji cha Mbalinyi na kuongeza kuwa baadhi yao tayari wameshapatiwa maeneo kwa ajili ya kuendeleza kwa kilimo na makazi.

Nao wananchi waliohamia Kijiji cha Biro kutoka Kijiji cha Ngombo wameishukuru Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwalipa fidia zao Kwa wakati ambazo zimewasaidia kuhama na kuanza maisha mapya katika vijiji jirani.

"Toka nitoke Kijiji cha Ngombo ambapo tuliondolewa kisheria kwakweli sina changamoto yoyote kimaisha, niko vizuri naishi vizuri na familia. Naishukuru Serikali, fidia nimepata kwahiyo mpaka hapa sina neno na Serikali" amesema Daudi Deodatus Lyambu aliyekuwa mkazi wa Ngombo ambaye sasa amehamia Kijiji cha Biro.

Ikumbukwe kuwa mnamo tarehe 17 Februari, 2023 Pori la Akiba Kilombero lenye sehemu A na B lilianzishwa kwa Tangazo la Serikali Namba 64 kufuatia kupandishwa hadhi kwa sehemu ya Pori Tengefu la Kilombero kuwa Pori la Akiba.

Aidha, kufuatia kuanzishwa kwa Pori la Akiba Kilombero, masharti na sheria zinazosimamia eneo hilo zilibadilika ambapo shughuli zote za kibinadamu zimesitishwa isipokuwa zile zinazokubalika kwa mujibu wa sheria. Lengo la Serikali likiwa ni kuimarisha usimamizi wa eneo hilo kwa kuhifadhi vyanzo vya maji, misitu na wanyamapori ili kuongeza tija ikiwemo upatikanaji wa maji kwa ajili ya uzalishaji wa umeme katika Bwawa la Mwl. Nyerere.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...