Skip to main content

FURAHIKA EDUCATION YAAHIDI KUINGA MKONO SERIKALI, YANADI MATUNDA YAKE


KATIKA kuelekea kutimiza miaka 48 ya Chama cha Mapinduzi (CCM),tangu kuzaliwa kwake, Chuo cha Ufundi Furahika VETA  kilichopo Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam kimeipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa kusimamia vyema ilani ya Chama hicho kwa kupiga hatua katika kukuza Sekta ya Elimu nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa bodi ya Chuo hicho Ngwenje Mohamed amesema Sekta hiyo imekuwa Kwa kiwango Cha juu ikilinganishwa na miaka ya huko nyuma kwani sasa shule za kata Kila mahali vyuo vya kati na vikuu vimeongezeka hiyo yote ni jitihada za Chama cha CCM kupitia ilani yake kuhakikisha kila Mtanzania bila kubagua dini Chama ukabila watu wote wanapata elimu.

"Kuelekea maadhimisho ya miaka 48 ya kuzaliwa chama cha CCM Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan tunaona mengi aliyoyafanya ameendeleza utoaji elimu bure vyuo vya Ufundi Veta navyo vikipewa kipaumbele ili kuibua ujuzi na tafitibalimbali hii inaonyesha  kuwa, mazingira ya Elimu nchini Tanzania ni mazuri "amesema Mohamed

Sambamba na hayo amebainisha kuwa ni mambo mengi yamefanyika  ikiwemo Sekta ya Afya ujenzi wa Zahanati kuongezeka kwa wataalamu wa Afya madaktari amesema kuwa tangu kuzaliwa kwa Chama hicho maendeleo ni makubwa ndani ya nchi ya Tanzania ikiwemo sekta ya uchumi unaku kwa kasi hospital, Shule, ambapo zamani wanafunzi walikua wakitumia umbali mrefu lakini sasa hivi kila Kata kuna zipo hata kiwango cha wasomi kinazidi kuongezeka pamoja na kuwepo kwa vyuo na vyuo vikuu nchini.

"Mazingira ya elimu yameboreshwa vizuri, sisi tunatoa elimu bure tena kwa viwango ambapo wanafunzi wetu waliohitimu zaidi ya 700 wamepata ajira katika sehemu mbalimbali, tuna kila sababu ya kuipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi bora na thabiti wa Dkt Samia"amesema

Aidha, amesema chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassani hata wao wadau wa maendeleo wameweza kuendesha vyuo na kutoa elimu bure, hiyo imetokana na Sera nzuri za Chama Cha Mapinduzi CCM pamoja utendaji kazi na ufualiaji ndio maana wamekua na uthubutu wa kukipongeza chama hicho.

Ameongeza kuwa mpaka sasa wanafunzi 1900 wameweza kupata elimu bure, ambapo hiyo imetokana na Sera nzuri za Chama cha Mapinduzi,huku wakipata wafadhili wa kuwalipia ada wanafunzi hali inayompunguzia majukumu mzazi kuweza kumpatia mtoto wake elimu ambapo jukumu lake ikiwa ni kumnunulia madaftari, peni na unform mtoto wake.

Hata hivyo, amesema wakati umefika wa kumuunga mkono Rais Dkt Samia kwa jitihada anazofanya ambapo kwa upande wa Zanzibar Rais Hussen Mwinyi ameleta mabadiliko makubwa ya kimaendeleo ikiwemo kuboresha miundombinu .

"Kutokana na matunda ya Chama Cha Mapinduzi sisi kama Taasisi ya Furahika tutaendelea kuinga mkono Serikali na kumuunga mkono Rais Dkt Samia, huku akiwapongeza wajumbe wa Chama hicho kwa kulipitisha jina la Rais Dkt Samia kugombea tena uchaguzi mkuu wa mwaka 2025"amesema Ngwenje.

Aidha, amesema kuwa Chuo hicho kinatoa elimu bure bila kuangalia mwanafunzi ametoka katika Chama gani wala dini yake wala kabila lake wanachokiangalia wao ni utayari wa mwanafunzi kuweza kupokea mafunzo na kwenda kuwafanyia kazi ili kujikwamua kiuchumi.

Hata hivyo, amesema katika kuharakisha maendeleo na kuwasaidia wazazi kuanzia mwezi wa tano wanafunzi watapewa chakula bure ili kuhakikisha wanapata elimu bora na kupata utulivu wa ajili pindi wanapokuepo darasani

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...