Skip to main content

RAIS SAMIA APONGEZWA KUWEZESHA UJENZI OFISI KUU WMA




✅Katibu Mkuu Viwanda na Biashara amshukuru Rais kutumia vyema fedha za Watanzania

✅Akagua ujenzi Jengo la WMA na kukiri kuridhishwa

✅Mtendaji Mkuu WMA asema litakamilika Februari 10

✅Litakuwa na Maabara ya kisasa yenye kuhifadhi vipimo kiwango cha kimataifa

 Na Veronica Simba – WMA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah amempongeza na kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kuwezesha ujenzi wa Jengo la Ofisi Kuu ya Wakala wa Vipimo (WMA) jijini Dodoma akisema ni matumizi mazuri ya fedha za Watanzania.

Ameyasema hayo leo Januari 20, 2025 baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo hilo ambalo limegharimu shilingi bilioni 6.2 na liko katika hatua za mwisho kukamilika.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Dkt. Abdallah amesema kuwa lengo la ujenzi wa jengo hilo ni kuhakikisha utoaji huduma katika sekta ya biashara hususan katika bidhaa zinazotoka viwandani unaboreshwa.

Akifafanua, amesema kuwa maboresho ya kutoa huduma bora katika sekta ya biashara na katika uendelezaji wa viwanda ni pamoja na kuwa na mazingira mazuri kwa wafanyakazi na yale ya utoaji wa huduma hizo.

“Na katika hili, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mambo mengi makubwa, mojawapo ikiwa ni ujenzi wa jengo hili ambalo tunakwenda kulizindua hivi karibuni,” amesisitiza.

“Ninyi wenyewe ni mashahidi; fedha za Watanzania zinaenda kukamilisha ujenzi huu ili tuweze kutoa huduma bora katika jamii ya wafanyabiashara ili tuweze kuleta maendeleo na tija katika sekta ya viwanda,” ameongeza Katibu Mkuu.

Kuhusu mtazamo wake kutokana na maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo, Katibu Mkuu Hashil ameeleza kuwa kwa mujibu wa maelezo na uthibitisho uliotolewa pamoja na kujionea kwa macho kazi inavyoendelea, ni dhahiri Mkandarasi atakamilisha kazi ndani ya muda ulioafikiwa ambao ni Februari 10 mwaka huu.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa WMA, Alban Kihulla, pamoja na kuunga mkono pongezi na shukrani kwa Rais Samia kuwezesha ujenzi wa jengo hilo, pia amebainisha kuwa ujenzi umefikia asilimia 95.2 na kwamba kukamilika kwake siyo tu kutaboresha mazingira ya wafanyakazi wa Wakala bali pia kwa Serikali kwa ujumla.

Akidadavua baadhi ya faida zitakazopatikana kutokana na kukamilika kwa jengo hilo, Mtendaji Mkuu ameeleza kuwa maabara ya kisasa ndani yake itawezesha kuhifadhi vifaa ambavyo kitaalamu vinajulikana kama vyenye usahihi wa kati au kwa lugha ya kigeni ‘secondary standards’

“Niwakumbushe tu kuwa, Wakala wa Vipimo ndiyo umepewa jukumu la kuhifadhi vipimo vyenye usahihi wa kati, kwa maana pale ndiyo tunalinganishwa kimataifa na ndipo unaleta ongezeko la imani kwa wawekezaji kuja kuwekeza nchini wakijua kwamba usahihi wa vipimo unafuatiliwa kutoka ngazi ya mfanyabiashara mpaka ngazi ya kimataifa.”

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, mwakilishi wa Mkandarasi anayejenga jengo hilo kutoka Kampuni ya Mohamed Builders, Bwana Burhan Hamza pamoja na Mshauri Elekezi kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST), Bi Rachel Lista wamethibitisha kuwa jengo litakamilika na kukabidhiwa kwa WMA Februari 10, 2025.

Ujenzi wa Jengo la Ofisi Kuu ya Wakala wa Vipimo, lililopo eneo la Medeli jijini Dodoma ulianza Julai 2, 2022 na matarajio ilikuwa likamilike Desemba 30, 2024 lakini Mkandarasi aliomba kuongezewa siku 40 kutokana na changamoto ndogondogo alizokutana nazo.

Hadi sasa Mkandarasi amelipwa jumla ya shilingi bilioni 5.8 kati ya shilingi bilioni 6.2 ambayo ni gharama ya utekelezaji wa Mradi huo.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...