Skip to main content

SHIRIKA LA POSTA LAZINDUA MFUMO WA USAFIRISHAJI VIFURUSHI

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry William Silaa (Mb), amesema kuwa kupitia mfumo wa usafirishaji wa vifurushi, mizigo, na abiria Serikali itaimarisha uchumi wa kidijitali, kukuza baishara mtandao na kuleta ajira nyingi kwa vijana hususan madereva wa pikipiki (bodaboda).  


Waziri Silaa ameyasema hayo  wakati akizundua mfumo wa usafirishaji wa vifurushi, mizigo, na abiria ujulikanao kama “Swifpack” na kusisitiza kuwa, huduma hii itatoa fursa za kipato cha uhakika, na kuifanya kazi ya bodaboda kuwa sawa na kazi nyingine za usafirishaji wa vifurushi, mizigo, na abiria.

"Leo tunashuhudia hatua nyingine muhimu kwa Shirika la Posta Tanzania kupitia huduma ya Swifpack ambayo itawezesha upatikanaji wa huduma za usafirishaji wa vifurushi, mizigo na abiria kwa kasi, ufanisi na gharama nafuu", amesema Waziri Silaa 

Ameongeza kuwa Teknolojia inabadilisha jinsi tunavyofanya kazi na kuwasiliana, na huu ni mfano bora wa jinsi taasisi za umma zinavyoweza kutumia ubunifu wa teknolojia kutibu mahitaji ya soko na kuboresha huduma kwa wananchi.  

Awali akitoa salamu za Shirika la Posta Tanzania, Postamasta Mkuu Macrice Mbodo amesema kuwa shirika hilo limeendelea kutekeleza mkakati wake wa nane wa biashara wenye dhamira ya kuifanya Posta ya Tanzania kuwa posta ya Kidijitali kwa biashara endelevu.



"Moja ya mafanikio tuliyoyapata kupitia utekelezaji wa mkakati huu, tumefanikiwa kuunganisha huduma na biashara zetu kwenye programu tumizi inayojulikana kama "posta kiganjani’ inayopatikana playstore na Apple store ambapo kwa sasa kupitia programu hii mwananchi yeyote mwenye simu janja anaweza kufurahia huduma zetu za posta kiganjani mwake ikiwemo kufuatilia mzigo wake (tracking), kuomba na kufanya malipo ya huduma zetu mbalimbali", amesema Mbodo.

Aidha, Waziri Silaa alieleza kuwa Serikali ina matarajio makubwa na kwamba huduma hii itachangia kubadilisha mtazamo wa jamii kuhusu kazi za bodaboda, ambazo mara nyingi zimekuwa zikipata sifa mbaya mitandaoni na kutajwa kwa changamoto mbalimbali za kijamii.



Waziri Silaa ameliagiza Shirika la Posta kuhakikisha kuwa linaimarisha mfumo wa ufuatiliaji wa mizigo na vifurushi (real-time tracking) unafanya kazi kikamilifu, kutoa taarifa sahihi kwa wateja na kuongeza ushirikiano na Sekta Binafsi ili kuhakikisha huduma hii inahudumia wananchi wengi na inafika maeneo mengi zaidi nchini.





Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...