Skip to main content

TAMASHA LA SAUTI ZA BUSARA KUTIKISA ZANZIBAR FEB 14 HADI 16



Na Mwandishi wetu

Wasanii kutoka Bara nzima la Afrika wanatarajia kujumuika kwa pamoja kuonesha vipaji vyao katika jukwaa la  Tamasha la Sauti za Busara linalotarajiwa kufanyika Februari 14 hadi 16 Ngome Kongwe Zanzibar huku liongozwa  na kauli mbiu ya "Voice For Peace".

Akizugumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa tamasha hilo,Journey Ramadhan  amesema tamasha hilo litafanyika kwa siku tatu za amani, umoja, ubunifu pamoja na utofauti .

"Tunawaalika wapenzi wa muziki na wafuasi wa amani kutoka pande zote za dunia kuungana katika tamasha hili kwa siku tatu hivyo tamasha la  Sauti za Busara 2025 linatarajiwa kuwa tukio lisilosahulika"amesema Ramadhan

Akitaja majina ya wasanii hao ni pamoja  Thandiswa(Afrika Kusini), Blinky Bill(Kenya), Christian Bella&Malaika Bendi (Tanzania), Bokani Dyer (Afrika Kusini) Frida Amani (Tanzania) The Zawose Queens,Kasiva Mutual,(Kenya) Zanzibar Taarab Heritage Ensemble(Zanzibar), Leo Mkanyia & Swahili Blues (Tanzania), Boukouru(Rwanda), Tryphon Evarist (Zanzibar), Charles Obina (Uganda) na Baba Kash(Tanzania).

Wengine ni Assa Matusse (Msumbiji), Mumba Yachi(Congo), Nidhal Yahyaoui (Tunisia), Etinsel Maloya (Reunion), WD Abo (Sudan) uKhoiKhoi(Afrika Kusini), Joyce Babatunde (Kamerun).

Vilevile amesema tamasha hilo pia litajumuisha maonesho ya kipekee ya mchana  yatakayofanyika Februari 15 katika mji wa Fumba Town mradi ulichini ya CPS Nyamanzi likitoa burudani huku jukwaa la Forodhani likiendelea kusisimua watanzamaji kwa mziki wa moja kwa moja ukitoa hamasa ya Amani, Umoja na fursa ya kusherekea utamaduni wa mwafrika.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Busara Promotions Lorenz Herrmann amesema wamekuwa wakitegeneza ajira zaidi 200 kupitia Tamasha la Sauti ya busara.

Aidha aliwashukuru wadau mbalimbali ambao wamekuwa wakishirikiana na Taasisi hiyo kwa kutumia nguvu ya muziki kuamasisha amani,maelewano pamoja na kuongeza uelewa kuhusu jukumu la kubadilisha jamii kupitia muziki.

Naye Mwakilishi wa wasanii watakaoshiriki katika Tamasha hilo, Leo Mkanyia amesema anafurahi kuwa mmoja washiriki katika tamasha la Sauti ya Busara 2025 huku akiwaalika wapenzi wa muziki kujitokeza na kuungana nao.

Aidha kiingilio hakuna ni bure usafiri hivyo wapenzi wa burudani wanaalikwa kutakuwa na maada mbalimbali zitakazoendeshwa ikiwemo kutokomeza ukatili wa.kijinsia

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...