Skip to main content

TMA YATOA USHAURI HUU KUELEKEA MVUA ZA MSIMU WA MASIKA


 Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania (TMA) imewataka watumiaji wa taarifa za hali ya hewa ikiwa ni pamoja na wakulima, wafugaji, mamlaka za wanyama pori, mamlaka za maji na Afya kuendelea kufuata, kupata na kuzingatia ushauri wa wataalam katika sekta husika ili kuepusha athari zinazoweza kujitokeza katika mvua za msimu wa masika.


Ushauri huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt Ladislaus Chang'a alipokua akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa mwelekeo wa mvua mvua za msimu wa Masika kuanzia Machi hadi Mei mwaka 2025 ambapo mvua hizo zinatarajiwa kuanzia wiki ya kwanza na pili katika maeneo ya Kanda ya Ziwa Victoria na Pwani ya kaskazini.

Aidha, kwa wiki ya pili na ya tatu mwezi Machi mwaka huu katika maeneo ya Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki ambapo ongezeko la Mvua linatarajiwa mwezi April 2025.

"Athari zinatarajiwa ni vipindi vya unyevu wa kuzidi kiasi pamoja na mafuriko vinaweza kujitokeza na kuathiri ukuaji w mazao hususani katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani, kina Cha majibkatika mito na mabwawa kinatarajiwa kuongezeka hivyo hatari ya mafuriko hususani katika maeneo yanayoathiriwa na mafuriko"amesema

Hata hivyo, amesema  Mvua za wastani hadi juu ya wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya nyanda za juu Kaskazini Mashariki pamoja na Mashariki mwa Mikoa ya Mara na Simiyu, aidha mvua za wastani hadi chini ya wastani zinatarajiwa katika maeneo ya Pwani ya kaskazini kaskazini mwa Mkoa wa kigoma na ukanda wa Ziwa Victoria.

Amesema mvua za Masika zinatarajiwa kuanza Machi 2025 katika maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua, hasa Kanda ya Ziwa Victoria, Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki, Pwani ya Kaskazini, na kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma.

Amesema Mwelekeo wa mvua za Masika 2025 kwa Kanda ya Ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara) pamoja na kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma, Mvua za Wastani hadi Chini ya Wastani zinatarajiwa, ambapo zitaanza Machi, wiki ya kwanza hadi ya pili, na kuisha Mei, wiki ya kwanza.

Aidha Pwani ya Kaskazini (kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro, Pwani, Dar es Salaam, Tanga na visiwa vya Unguja na Pemba) Mvua za Wastani hadi Chini ya Wastani zitaanza Machi, wiki ya kwanza hadi ya pili, na kuisha Mei, wiki ya tatu hadi ya nne.

Pia Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro), kutakuwa na Mvua za Wastani hadi Juu ya Wastani ambapo zitaanza Machi, wiki ya pili hadi ya tatu, na kuisha Mei, wiki ya kwanza.

Amesema athari zinazotarajiwa ni pamoja na unyevu na mafuriko, ambapo Mvua nyingi zinatarajiwa katika baadhi ya maeneo, na huenda zikapelekea mafuriko na kuathiri ukuaji wa mazao.

Amesisitiza kuwa taarifa hiyo inatolewa kwa ajili ya kusaidia wadau wa sekta mbalimbali, kama vile kilimo, mifugo, uvuvi, maliasili, afya, nishati, usafirishaji, na usimamizi wa maafa, kuchukua tahadhari stahiki na kupanga mikakati ya kukabiliana na athari za mvua.

Awali alisema Mwenendo wa mvua za Msimu (Novemba 2024 – Aprili 2025) zinatarajiwa kuwa za Wastani hadi Chini ya Wastani katika mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi, Rukwa, Songwe, Singida na Dodoma, huku mvua za Wastani hadi Juu ya Wastani zikitarajiwa katika mikoa ya Njombe, Ruvuma, Mtwara, Lindi na mikoa mingine

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...