Skip to main content

WASIRA: UAMUZI WA MKUTANO MKUU UMEZINGATIA KATIBA YA CCM



Awapa darasa wanaodai sababu ya CCM kupitisha wagombea Urais

- Asema yupo tayari kuwapa somo waifahamu vyema katiba ya Chama  



MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mainduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, amesema uamuzi wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM, uliomchagua Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kugombea kiti cha Urais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, umezingatia takwa la kikatiba na mamlaka ya Mkutano Mkuu.

Amesema baadhi ya watu wanaojiita wanaCCM wanaodai kwamba bado hawajaelewa sababu ya wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM kupitisha uamuzi huo, atawasaidia kuelewesha kwani uwezo wa binadamu kufahamu jambo hauwezi kulingana.



Wasira aliyasema hayo jijini Dar es Salaam leo wakati viongozi, wanachama,  wapenzi wa CCM na wananchi kutoka maeneo mbalimbali walipojitokeza kumpokea.

"Baada ya Mkutano Mkuu kutambua kazi kubwa zilizofanywa na serikali zote mbili, Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar, Mkutano Mkuu wa CCM ukasema kama hali ni hii kuna sababu gani kuchelewesha kutangaza mgombea?.



"Sasa wapo watu wanaosema wao ni wanachama wa CCM, hawakuelewa. Hilo nalo siyo jambo la ajabu. Tutawasaidia kuelewa maana siyo watu wote wanaweza kuelewa sawa. lakini tunawaambia Mkutano Mkuu kwa mujibu wa Katiba ya CCM ndiyo kikao kikuu cha mwisho," amesema.

Wasira ameeleza kuwa Mkutano Mkuu wa Chama una mamlaka ya kubadili, kufuta na kurekebisha uamuzi wowote uliofanywa na kikao cha chini yake, kufuta maamuzi yaliyofanywa na kiongozi yeyote wa CCM.



Amesisitiza: "Sasa aliye na mashaka katika jambo hilo kama wote hawawezi aje kwangu nitamsadia maana katiba ipo kichwani. Uamuzi tulioufanya umezingatia Katiba ya CCM ibara ya 101 inayotutaka tuchague jina moja la kuwa mgombea wa kiti cha Urais, tulitumia ibara hiyo na kwa mamlaka ya Mkutano Mkuu ameteuliwa Dk. Samia."

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...