Skip to main content

CHUO CHA BAHARI DAR ES SALAAM (DMI) KUTOA MAFUNZO YA MANUFAA YA UCHUMI WA BULUU KWA VIJANA


Na Mwandishi wetu 

Mkuu wa chuo cha Bahari Dar es Salaam Prof. Tumaini Gurumo amesema kuwa chuo cha bahari Dar es Salaam (DMI) kimeona kunafursa nyingi katika uchumi wa buluu hivyo kinatazamiwa kuanzisha mafunzo ya muda mfupi na mrefu kwa vijan kusiana na manufaa katika uchumi wa  buluu.

Prof. Gurumo ameyasema hayo kwenye kongamano la uchumi wa buluu lilifanyika jiji Banjul nchini Gambia.

“Kweli  katika kongamano hili tumakubaliana nchi zote za Afrika kutumia vyanzo vyetu vya maji kama vila bahari, mito mabwa, maziwa na vyanzo vingine kuhakiisha vinasaidia jamii za kiafrika hivyo sisi DMI tutaanzisha masomo kwa vijana kuonyesha fursa za Uchumi wa Buluu” Asema Gurumo

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Uchukuzi Bi Stella Katondo amesema kuwa kongamo hilo limewakutanisha wataalam  kutoka nchi zaidi ya kumi na Sita za Afrika ni muhimu sana kwa maendeleo na manufaa ya uchumi wa buluu. Hivyo kwa chuo cha DMI imepata nguvu ya kuendelea kutoa elimu ya umuhimu wa uchumi wa buluu.

Naye mkurugenzi wa Usalama na Mazingira kutoka shirika la uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bi. Leticia Mutaki amesema kuwa kupitia kongamano hilo TASAC itaendelea na kazi ya kudhibiti uchafuzi wa mazingira katika vyanzo vya maji ili viumbe walipo waendele kuishi kwa manufaa ya mazingira na wananchi.

Katika Kongamano lilifanyika kwa siku tatu liliwakutanisha wataalamu kutaka nchi zaidi ya kumi na sita walikubaliana kushirikiana katika kuweka nguvu ya pamoja kuona kwa namna gani vyanzo vya maji vilivyopo Afrika vina wanufaisha wanchi wote wa Afrika.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...