Skip to main content

HIKI NDICHO ALICHOKISEMA DIWANI SHABANI KUHUSU MNADA WA PUGU,WADAU KUCHANGIA UJENZI WA OFISI


LICHA ya kufanya harambee kwa ajili ya kujenga ofisi ya wafanyabiashara wa Pugu Mnadani imeelezwa kuwa kuna Changamoto ya wafanyabiashara kupeleka ngo'mbe zao moja moja kwa moja kwenye machinjio bila kuzitisha kwenye Mnada hali inayochangia kurudisha nyuma maendeleo ya Mnada mkuu wa Pugu.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya harambee hiyo, jijini Dar es Salaam, Diwani wa Kata ya Pugu Stesheni Shaban Mussa amesema kwa sasa mzunguko wa fedha umeshuka katika Mnada huo kutoka shill Bill 1.2 kwa siku hadi kufikia shill mill 800.

Amesema kuwa, kuna wafanyabiashara ambao sio waamini wanabeba mifugo kutoka mikoa mbalimbali hawaifikishi Mnadani na kupeka machinjioni moja kwa moja ambapo kisheria mifugo yote inatakiwa kufika mnadani hapo washushe ili wanunuzi wanunue na kwenda kuchinjwa machinjioni. 



"Wanapopeleka ngo'mbe moja kwa moja machinjioni sisi hapa hatuwezi kupata fedha kwani sheria za machinjio haziruhusu kukusanya ushuru ngo'mbe zikiwa nzima, bali ni mifugo iliyochiniwa tu"amesema

Ameongeza kuwa, wameweka mikakati na mkuu wa minada pamoja na kuzungumza na viongozi wenzake kuhakikisha ngo'mbe zote zinazofika machinjio lazima zuwe na vibali ambayo vimesaini kutoka Mnada mkuu wa Pugu.


Aidha, amesema watakaa na wafanyabiashara kuwaeleza umuhimu wa kulipa kodi kwani changamoto zilizopo Mnadani hapo haziwezi kutatulika kama wao hawalipi kodi na maendeleo hayawezi kupatikana.

"Hapa tumesikiliza changamoto zao wanataka maji, barabara, taa lakini haya yote hayawezi kufanyika bila wao kulipa kodi, mapato yakikusanywa lazima maendeleo yaonekane"



Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Pugu Mnadani Edward Ntemi amesema kuwa, kulichomsukuma kuanzisha harambee za ujenzi wa ofisi ya wafanyabiashara wa Pugu Mnadani na kushirikisha wadau ni changamoto za wafanyabiashara, ikiwemo kukosa sehemu maalum ya kukutana na kutatua changamoto zao kwa faraghaa, kwani kwa sasa wanakutana popote.



"Nilipochaguliwa mwaka 2024 niliahidi wapiga kura wangu nitafanya sherehe kuwa nitachinja ngo'mbe ili tule nyama lakini nikafikiria nyuma kwa hayyat Magufuli alivokuwa akifanya pesa za  sherehe za uhuru akizihamishia kwenye ununuzi wa vitanda vya hospital, sisi hapa hatuna ofisi nikaona ni bora pesa hizi nizihamishie kwenye kwenye ujenzi wa ofisi" amesema Ntemi.

"Mfano mwezi unaokuja wa mfungo wa Ramadhani wageni wanaweza kufika na tukapewa tenda ya kusaply hata ngo'mbe 200 kama hatuna ofisi itakua ni changamoto.



Aidha, amewataka wadau mbalimbali waendelee kuwaunga mkono kwa kushirikiana na wanachama pamoja na viongozi wenzake wanamkakati wa kuanzisha vyanzo mbalimbali vya mapato, huku akiwataka wafanyabiashara hao kujiunga pamoja Kwa kujisajili ili wafahamike hata inapotekea jambo iwe rahisi kutatulika.



Naye, Meneja Mkuu wa Mnada Mkuu wa Pugu Noely Byamungu amezitaka Taasisi za kifedha kwenda kuekeza Mnadani hapo na kutoa elimu ya usimamizi wa fedha kwani fedha inayopatikana kwa siku Mnadani hapo ni kati mill 800 hadi Bill 1 lakini maisha ya wafanyabiashara hao  hayaendani na mzunguko wa fedha hiyo.

"Mzunguko wetu wa fedha hapa ni mkubwa sana lakini maisha ya wafanyabiashara hapa hayaendani na uhalisia wa pesa wanayoipata kutokana na kukosa usimamizi mzuri wa fedha"

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...