Skip to main content

MAMA SAMIA LEGAL AID YAFIKIA WANANCHI ZAIDI YA MILIONI 1-MAJALIWA






_Asema kampeni hiyo ni ubunifu wa Rais Dkt. Samia ya kuwasaidia Watanzania wasio na uwezo kupata huduma za kisheria bure._

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia ni ubunifu wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan uliolenga kuongeza wigo wa upatikanaji haki kwa wananchi wasio na uwezo wa kumudu gharama za huduma za kisheria.

Amesema kuwa kupitia kampeni hiyo ambayo inatolewa bure mpaka sasa imefanikiwa kuwafikia zaidi ya wananchi milioni moja wakiwemo wanawake 681,326 na wanaume 691,773 katika mikoa 19 nchini.

Amesema hayo leo Jumatano (Februari 19, 2025) wakati alipozindua kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia katika mkoa wa Lindi, kwenye viwanja vya Madini, Ruangwa Mkoani Lindi.

“Mheshimiwa Dkt. Samia alijifunza shida, kero na changamoto wanazopata watanzania na hasa wale ambao hawana uwezo wa kulipia gharama za huduma za kisheria, aliguswa na akaamua kuanzisha kampeni hii na kuikabidhi Wizara ya Katiba na Sheria isimamie”

Ameongeza kuwa kupitia kampeni hii migogoro mbalimbali ya ardhi, ndoa, mirathi imetatuliwa. Ni ukweli isiopingika kuwa, jamii nyingi zimekuwa na changamoto kuhusu mirathi ambazo zinachangia kuondoa amani miongoni mwa wanandugu kwa kugombania mali.”

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa wakuu wa wilaya nchini kuweka mpango wa kufanya ziara kwenye maeneo yao wakiwa na wanasheria ili kusikiliza na kutatua kero za kisheria za wananchi badala ya kusubiri viongozi wa kitaifa. “Watanzania wanahitaji huduma ya Serikali hii na Serikali imefanya kazi kubwa sana kwenye nchi hii na bado tumeahidi kuwatumikia”

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa, pamoja na kampeni hiyo, Rais Dkt. Samia amefanya mageuzi makubwa na kuweka kipaumbele katika kutatua changamoto zilizopo sekta ya huduma za sheria nchini.

Pia, Mheshimiwa Majaliwa ameiagiza Wizara ya Katiba na Sheria kupitia Ofisi ya Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini RITA kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kuandika na kutunza wosia na kugawa mirathi kwa mujibu wa sheria ili kupunguza migogoro miongoni mwa wanafamilia.

Naye, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Palamagamba Kabudi amesema kuwa kampeni ya msaada wa kisheria ya mama Samia unasifa nne ambazo ni umuhimu wake kwa jamii, umaalum wake ni kwasababu inatelekeza maelekezo ya Rais Dkt. Samia, umahususi wake imeasisiwa na Rais Dkt. Samia “ukipekee wake ni kwasabau inatekeleza falsafa ya R4”

Kwa Upande wake Naibu Waziri Katiba na Sheria Jumanne Sagini amesema kuwa Wizara ya Katiba na Sheria inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha wananchi wanaifikia haki kwa wakati na kwa ufanisi.

Amesema kuwa ili kuhakikisha lengo hilo linawezekana, Wizara imeendela kutoa mafunzo kwa wasaidizi wa kisheria na kujenga uwezo kwa watoa huduma za msaada wa kisheria ili kuendelea kusogeza zaidi huduma hizo karibu na wananchi. 

“Mwezi Desemba, 2024, Wizara iliingia makubaliano na Chama cha Wanasheria Tanganyika kwa lengo la kuimarisha zaidi huduma za uwakili kwa wananchi wasiokuwa na uwezo wa kumudu gharama za mawakili”

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...