Skip to main content

MHE. BITEKO AMPONGEZA MWANAFUNZI ALIYEELEZEA MIRADI YA UMEME

 





 Amuahidi kutembelea mradi wa Julius Nyerere        

Na Josephine Maxime- Dar es Salaam           

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mheshimiwa Dkt. Doto Biteko ameagiza Mwanafunzi Mirabelle Msukari na Wenzake wa Shule ya Msingi Sun Rise iliyopo Wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam kupelekwa katika Mradi wa kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) ili kujifunza zaidi kwa Vitendo namna mradi huo unavyozalisha Umeme.

Mheshimiwa Biteko amesema  hayo leo Februari 18 kwa njia ya simu baada ya Naibu Waziri wa Nishati Mheshimiwa Judith Kapinga  kutembelea shule hiyo kwa lengo la kumpongeza mwanafunzi huyo ambaye video yake ilijizolea umaarufu kupitia mitandao ya kijamii ambapo  Mirabelle alielezea kwa ufanisi juu ya miradi mbalimbali ya umeme inayotekelezwa nchini ukiwemo mradi wa Julius Nyerere.

‘’Sisi tukupongeze na tumefurahi kwa umri wako unafuatilia masuala ya Nishati, sasa tutakupeleka kuliona Bwawa la Julius Nyerere uone Umeme unavyozalishwa ili uendelee kujifunza zaidi. Sisi tunatamani kukuona ukifanikiwa zaidi,” amesema Mhe. Biteko

Kwa Upande wake Naibu Waziri wa Nishati Mheshimiwa Judith Kapinga amesema Miradi hii ya kimkakati ambayo inatekelezwa nchini ni jitihada za Serikali chini ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dokta Samia Suluhu Hassan ambaye ameonesha dhamira ya dhati  kuendeleza miradi ya umeme nchini ukiwemo mradi wa JNHPP ambao kwa sasa umefikia asilimia 99.8.

“Wakati Mheshimiwa Rais anaingia madarakani, Mradi wa Julius Nyerere ulikuwa asilimia 33, leo tunavyozungumza umefikia zaidi ya asilimia 99 na mashine nane tayari zimeingizwa kwenye gridi ya Taifa. Imebaki mashine moja pekee ambapo mradi uko mbioni kukamilika,” amesisitiza mheshimiwa Kapinga

Nae Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa wateja Bi. Irene Gowelle akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) , amesema wamepokea kwa vitendo agizo la Mheshimiwa Dkt. Biteko la kuhakikisha mwanafunzi huyo anafanya ziara katika Mradi wa Julius Nyerere ambapo pia amefafanua kuwa elimu na taarifa zinazotolewa na TANESCO zinawafikia walengwa kwa usahihi.

“Hatua hii inatupa nafasi ya kuona kwamba elimu na taarifa mbalimbali tunazozitoa zinawafikia moja kwa moja makundi mbalimbali i?wakiwemo  watoto na ndio maana mmeweza kuona Mirabelle akizungumza kwa ufasaha.

Sisi kama Shirika la Umeme tutaendelea kufanya hivyo” amefafanua Bi. Gowele.

Mwanafunzi huyo  licha ya pongezi ,amepewa zawadi mbalimbali ikiwemo Komputa Mpakato (Laptop) pamoja na fedha kiasi cha Shilingi Milioni Mbili.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...