Skip to main content

NLD YAJIWEKA MGUU SAWA NA UCHAGUZI MKUU



Chama cha National league for Democracy kimesema kimeanza kujiweka mguu sawa katika maandalizi ya uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika hapo badae.

Akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari Makao Makuu ya chama hicho, Tandika jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Chama cha National League for Democracy (NLD), Mhe. Doyo Hassan Doyo, alielezea hatua zinazochukuliwa na chama hicho kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

.Doyo alisema kuwa chama hicho kimeanza kufanya vikao mbalimbali vya tathmini ya Uchaguzi uliopita, hususan Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, vijiji, na vitongoji, huku lengo kuu likiwa ni kujiandaa kikamilifu kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu. Aliongeza kuwa tathmini hiyo inalenga kubaini namna chama hicho kitakavyoshiriki katika uchaguzi huo mkubwa na kuhakikisha kuwa hakikosi nafasi yake katika ulingo wa siasa.

Pamoja na kukutana na changamoto katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, vijiji, na vitongoji, Katibu Mkuu wa NLD alisisitiza kuwa hilo halitakuwa kikwazo kwa chama hicho kushiriki katika Uchaguzi Mkuu. Alisema, "Kwa wale ambao wana sababu za kususa, na wasuse, lakini Chama cha National League for Democracy (NLD) hakiwezi kumuachia nguruwe shamba la miogoo. NLD tutashiriki uchaguzi mkuu kwa kiwango kile kile mpaka dunia ijuwe kwamba haki yetu inapokonywa hapa."

Chama cha NLD kimeendelea na vikao vya kikanuni, lengo likiwa ni kupata wagombea wanaokubalika katika jamii kwa ajili ya nafasi za Ubunge, Urais, na Udiwani. Maandalizi ya chama hicho yanaendelea kwa kasi huku viongozi wakiwa na dhamira ya kuhakikisha kuwa uchaguzi wa Oktoba mwaka huu unakuwa na uwakilishi bora kutoka NLD.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...