Skip to main content

OPARESHENI YA KUWADHIBITI FISI SIMIYU YAONESHA MAFANIKIO MAKUBWA




📍 Zaidi ya Fisi 16 wavunwa.

Na Mwandishi wetu, Simiyu.

Oparesheni maalumu ya kuwadhibiti wanyamapori wakali na waharibifu aina ya fisi waliokuwa wanaleta taharuki na madhara Kwa jamii inayoendelea Mkoani Simiyu imeonesha mafanikio makubwa baada ya fisi 16 kuvunwa ikiwa ni hatua muhimu iliyochukuliwa na Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii ya kuhakikisha usalama na utulivu Kwa wananchi vinarejea.

Hayo yamesemwa leo Februari 19, 2025 na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Kenani Kihongosi alipokuwa akiongea na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari.

Mhe. Kihongosi amesema kufuatia changamoto hiyo,  Serikali ilichukua jukumu kubwa la kuhakikisha inalinda wananchi wake ikiwemo kuanzisha oparesheni maalumu inayohusisha Jeshi la Uhifadhi Kwa Taasisi za TAWA, TANAPA na TFS Kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi pamoja na wananchi, oparesheni inayotajwa kuanza  Januari 25, 2025.

"Tarehe 20/12/2024 baada ya fisi kuvamia wananchi Serikali ilichukua hatua kubwa ya kushirikisha vyombo vyake (TAWA na Jeshi la Polisi) na kuanza Oparesheni, lakini ilipofika tarehe 25/01/2025 oparesheni ya mkoa mzima ilifanyika Kwa ukubwa kuhakikisha inakabiliana na fisi wote waliokuwa wanasumbua wananchi" amesema Mhe. Kihongosi 

"Na Kwa taarifa njema ni kwamba tangu kuanza Kwa oparesheni hii vyombo vyetu vimeweza kudhibiti na kuua fisi 16 na ndio maana kwasasa mnaweza kuona hali imetulia" ameongeza Mkuu huyo wa mkoa wa Simiyu.

Aidha Mhe. Kihongosi ameendelea kuwatoa hofu wananchi wa mkoa huo akisisitiza kuwa hali ni shwari na kuwataka waendelee na shughuli zao kama kawaida huku akikemea vikali imani za kishirikina kuhusiana na mnyamapori aina ya fisi kwa baadhi ya wakazi wa Simiyu na kuwataka wote wanaofuga wanyamapori pori hao kuacha mara moja kwani ni kosa kisheria kumiliki nyara za Serikali bila Kibali.



Kwa upande wake Afisa Habari wa TAWA Beatus Maganja amewaomba wananchi wa Mkoa wa Simiyu hususani wilaya ya Itilima kuacha tabia ya kutembea  nyakati za usiku na alfajiri kwani ni nyakati ambazo wanyama fisi huwa katika mawindo yao.

Vilevile amewasisitiza wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Maofisa wa Jeshi la Uhifadhi waliopo uwandani ili kuongeza ufanisi wa zoezi hilo huku akiwahakikishia  kuwa Serikali imedhamiria kulinda wananchi wake na kwamba Askari wapo uwandani wanafanya Kazi usiku na mchana kuwahakikishia usalama wao.

Kwa upande wao wananchi wa Simiyu hususani wilaya ya Itilima wameshukuru Kwa juhudi zinazofanywa na Serikali katika kukabiliana na changamoto hiyo, wakisema kuwa hatua hiyo imeweza kuwarejeshea matumaini, utulivu na amani.

"Kwakweli tulikuwa tunasumbuliwa sana na haya mafisi ambayo yalikuwa yanauma watu, baada ya Serikali kusikia ikaweka ulinzi, kwakweli imetufanyia vizuri sana mpaka leo hatujawasikia tena tangu Askari waanze kuwashambulia hao fisi, mpaka leo hii tuna utulivu sana kwakweli tunashukuru sana"   amesema Mozo Mabula  mkazi wa Kijiji cha Mwamunhu kilichopo wilaya ya Itilima.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...