Skip to main content

UJENZI KITUO CHA KUPOZA UMEME HANDENI KUIMARISHA UPATIKANAJI UMEME- RAIS SAMIA





Kituo  kugharimu  shilingi bilioni 50

Zaidi ya Shillingi billioni 98 kutekeleza mradi wa gridi imara Kilindi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema utekelezaji wa ujenzi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Handeni mkoani Tanga  utakapokamilika utaboreha upatikanaji wa umeme katika Wilaya za Handeni  na Kilindi pamoja na maeneo jirani.

Rais Samia ameyasema hayo leo Februari 25, 2025 katika ziara yake mkoani Tanga wakati akizungumza na wananchi wa Handeni mara baada ya kuzindua Shule ya Wasichana ya Kilindi na Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni. 

"Tatizo la umeme hapa Handeni Serikali inalifahamu, imeanza kuchukua hatua kwa ujenzi wa kituo cha kupoza umeme   kitakachogharimu takribani  shilingi  bilioni 50 za kitanzania ambacho kitaboresha upatikanaji wa umeme." Amesema Rais Samia

Ameeleza kuwa,  upatikanaji wa umeme wa uhakika Handeni utasaidia ukuaji wa uchumi pamoja na kuyainua madini ya kinywe ambayo yanapatikana Wilaya ya Kilindi na yanahitaji umeme wa kutosha.

Awali,  Mbunge wa Kilindi, Mhe. Omari Kigua aliishukuru Serikali  kwa niaba ya wananchi kwa kutoa zaidi ya shilingi bilioni 98 kwa ajili ya kutekeleza mradi ya gridi imara utakao husisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Mkata kupitia Handeni  hadi Kilindi. 

Mhe. Kigua ameeleza kuwa Wilaya ya Kilindi ina Vijiji 102 ambavyo vyote vimefikiwa na umeme na sasa kazi inayoendelea ni ya kufikisha umeme kwenye Vitongoji.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...