Skip to main content

KAPINGA AZINDUA NAMBA YA BURE YA HUDUMA KWA WATEJA WA TANESCO


Awapongeza TANESCO kutekeleza agizo la Mhe. Dkt. Biteko kuwataka kuanzisha namba ya huduma kwa wateja bure

 Asema namba hii ya 180 ya bure kwa wateja kuimarisha huduma kwa wateja na kutatua changamoto zao

Awaagiza Mameneja wa Mikoa na wilaya wa TANESCO kuwasimamia watoa huduma

Awaasa watanzania kutumia namba hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa na si vinginevyo



Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga leo Machi 12, 2025 amezindua namba mpya ya huduma kwa wateja (mchongo 180) itakayotumiwa na wateja bure bila malipo ili kupata huduma mbalimbali kupitia kituo cha miito ya simu cha Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Kuanzishwa kwa namba hiyo inafuatia agizo lililotolewa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko la kuwataka TANESCO kuhakikisha wanakuwa na namba ya bure bila malipo kwa wateja ili kuboresha utoaji huduma kwa wateja na kupunguza malalamiko yasiyo ya lazima na kuongeza wigo wa wapokeaji wa simu kutoka namba ya awali hadi 150 kwa awamu.



‘’Naomba  niwahakikishie kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais  Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imekusudia watanzania wapate umeme  wa uhakika na kuongeza kuwa Wizara ya Nishati itaendelea kuisimamia TANESCO na taasisi nyingine chini ya  Wizara kuhakikisha sekta ndogo ya umeme  inakuwa na kuleta maendeleo kwa Watanzania.

 Awali akizungumza kabla ya mgeni rasmi, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO,  Balozi Zuhura Bundala amesema mapinduzi kwenye utoaji huduma kwa wateja ni moja ya masuala ya kipaumbele ili kuchochea uchumi wa Nchi na kuongeza kuwa shughuli za uchumi zinategemea sana uwepo wa umeme wa kutosha na uhakika na ndio maana bodi imejipanga kutekeleza maagizo mbalimbali yanayotolewa na Wizara.



Amesema bodi iko tayari kuhakikisha TANESCO inafanya kazi kwa bidii na jkutoa huduma bora kwa wateja ili kupunguza kero na changamoto za masuala mbalimbali.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mha. Gissima-Nyamo Hanga amesena dunia ya sasa ya biashara na ushibdani wa kibiashara unategemea uwepo wa huduma bora ya uneme na kutatua changamoto kwa wakati



Aidha, Mha. Gissima amesema licha ya kujipanga kutoa huduma bora kwa wateja pia wamekuwa wakitekeleza kwa vitendo uhamasishaji wa matumizi bora ya nishati kwa kutumia umeme.

Hafla hiyo imehudhuriwa na wawakilishi kutoka Wizara ya Nishati, bodi ya wakurugenzi ya TANESCO na wadau mbalimbali



Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...