Skip to main content

KUELEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI


Wizara ya Nishati yajivunia jitihada katika kulinda haki, usawa na kuwawezesha wanawake

Kapinga asema lengo ni kuboresha ustawi wa mwanamke na kuongeza thamani yake.

Katika kuelekea maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani Machi 8, 2025, yenye kaulimbiu "Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji” Wizara ya Nishati inajivunia jitihada zinazofanyika nchini katika kulinda haki usawa na kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia nishati ya umeme na nishati safi ya kupikia. 

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri Nishati, Mhe. Judith Kapinga alipokuwa akieleza ni nama gani Wizara ya Nishati inakwenda kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.

"Tumepeleka umeme kwenye zaidi ya Vitongoji elfu 33, lakini kupitia nishati safi ya kupikia kupitia programu mbalimbali tumepeleka mitungi takribani laki 4020, majiko banifu laki 2 pamoja na majiko ya umeme." Amesema  Kapinga 

Ameeleza kuwa jitihada zote za Serikali katika  uwekezaji sekta ya nishati hususani nishati safi ya kupikia zinalenga kuboresha ustawi wa mwanamke na kuongeza thamani yake katika kujihusisha na shughuli za maendeleo katika jamii.

Aidha, Mhe. Kapinga amesema kuwa kupitia Sera ya Elimu Bure kumekuwa na ongezeko la dadi ya wanafunzi wa kike mashuleni, aidha uboreshaji katika sekta ya afya umewafanya wanawake wapate uhakika wa kuendelea na shughuli za uzalishaji kutokana na upatikanaji wa matibabu sahihi.

Amempongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa tuzo ya Golkeeper ambayo imetambua mchango katika kupungiza vifo vya kina mama wakati wa kujifungua kwa asilimia  80 na Vifo vya watoto chini ya miaka 5 kwa kila vizazi 1,000.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...