Skip to main content

PROF LIPUMBA ATOA RAI HII KWA SERIKALI

 


Na wandishi wetu 

Chama cha Wananchi (CUF) kimeitaka Serikali kupitia hotuba za bajeti ya mwaka huu kuchambua sababu za nini haifikii malengo ya Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama hicho Prof. Ibrahim Lipumba Wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juu ya mtazamo wa CUF kuhusu Bajeti ya Mwisho ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo 2021/22 hadi 2025/26.

Amesema kuwa kikao cha Bunge la Bajeti kinatarajiwa kuanza Aprili 8, 2025 na kwamba hii itakuwa Bajeti ya mwisho ya utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo 2021/22 – 2025/26 na mwaka wa mwisho wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, bajeti za Serikali zilizopita hazijajikita katika utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo. 

Prof. Lipumba amebainisha kuwa utaratibu wa zamani wa hotuba za Bunge la Bajeti ulianza na hotuba za Waziri wa Mipango na Waziri wa Fedha kueleza hali ya uchumi na utekelezaji wa mipango ya maendeleo na mapendekezo ya mapato na matumizi. 

"Hivi sasa Hotuba hizi ni za mwisho katika Bunge la Bajeti. Anayefungua dimba ni Waziri Mkuu ambaye anaeleza utekelezaji wa mipango ya Serikali kwa ujumla. Ili kuwatendea haki Watanzania Hotuba ya Waziri mkuu ianze kutoa ufafanuzi wa kwa nini Malengo ya Mpango wa tatu wa Maendeleo hayatafikiwa," amesema Prof. Lipumba na kuongeza,

"Mawaziri wa Sekta pia wajikite katika kuwaeleza Watanzania kushindwa kwa Serikali kutekeleza Mpango wa Tatu wa Maendeleo katika sekta zao,".

Ameeleza kuwa, katika Hotuba za bajeti Waziri mara kwa mara hueleza “Bajeti ya Serikali imeandaliwa kwa kuzingatia: Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025; Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya Mwaka 2020, Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2021/22 - 2025/26), Dira ya Maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki 2050, Ajenda ya Maendeleo ya Afrika 2063, Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030; pamoja na nyaraka, miongozo na makubaliano mengine ya kikanda na kimataifa ambayo Tanzania imeridhia."

Alibainisha kuwa Machi 11, 2025, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, aliwasilisha Bungeni mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2025/26. 

Hata hivyo, Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba, naye aliwasilisha Bungeni, Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2025/26 ambapo Serikali inapanga kukusanya na kutumia jumla ya shilingi trilioni 57.04 kwa mwaka 2025/26, sawa na ongezeko la asilimia 13.4 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka wa fedha 2024/25 ya shilingi trilioni 50.29.

Serikali inatarajia kukusanya shilingi trilioni 40.97 kutoka vyanzo vya ndani, ikiwa ni asilimia 69.7 ya bajeti yote ambapo Shilingi trilioni 16.07, sawa na asilimia 30.3 ya bajeti, zinatarajiwa kupatikana kupitia mikopo ya ndani na nje. 

"Badala yake Waziri wa Fedha ametumia Mfumo uliopendekezwa na Shirika la Fedha la Kimataifa – IMF la namna ya kuwasilisha Takwimu za Fedha za Serikali. Ni vyema wakati wa kuwasilisha bajeti Bungeni, Waziri atumie mifumo yote miwili kwani uchambuzi wa bajeti katika nchi zinazoendelea umejikita katika kubainisha bajeti ya matumizi ya kawaida na bajeti ya maendeleo," alieleza Prof. Lipumba

Ameongeza"Hotuba ya Waziri wa Fedha iliyowekwa kwenye tovuti ya Bunge na tovuti ya Wizara ya Fedha ni ya PDF iliyowekewa usimbaji fiche (encryption) kwa hiyo huwezi kutengeneza nakala ya hotuba kwa mfumo wa word au excel ili kurahisisha uchambuzi wa bajeti. Namshauri Waziri wa Fedha asitumie usimbaji fiche kwenye nakala ya Hotuba yake ya Bajeti na kwenye Vitabu vya Bajeti,"

Prof Mkumbo ameeleza kuwa Serikali imetenga TSh trilioni 19.47 kwa miradi ya maendeleo, ikiwemo TSh trilioni 13.32 kutoka vyanzo vya ndani na TSh trilioni 6.15 kutoka nje ambapo Matumizi kwenye miradi ya maendeleo yanatarajiwa kuwa asilimia 34.1 ya matumizi yote ya serikali.

Hata hivyo Waziri wa Fedha alieleza Malengo ya Uchumi Jumla kuwa ukuaji wa uchumi kufikia asilimia 6 mwaka 2025 kutoka asilimi 5.4 mwaka 2024Mfumko wa bei kuwa kati ya asilimia 3.0 – 5.0 

Mapato ya ndani kufikia asilimia 16.4 ya Pato la Taifa mwaka 2025/26 ukilinganisha na matarajio ya asilimia 15.8 mwaka 2024/25 ambapo mapato ya kodi kufikia asilimia 13.1 ya Pato la Taifa mwaka 2025/26 ukilinganisha na matarajio ya asilimia 12.8 mwaka 2024/25.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...