Skip to main content

RC CHALAMILA AFANYA ZIARA KIBAMBA, ATOA MAAGIZO HAYA






Na Mwandishi wetu Dar 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert  Chalamila ameahidi kutoa shilling mill 100 kwa ajili ujenzi wa Zahanati ya Saranga kupitia ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ubungo.

Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam wakati alipokua katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Jimbo la Kibamba sambamba na kuskiliza kero za wananchi ikiwemo afya, maji, barabara pamoja na Tasaf.

Amesema kuwa, licha ya Rais Dkt Samia kutoa fedha nyingi kwa ajili ya sekta ya Afya kwa kujenga hospital kubwa, kuongeza madaktari bingwa na kuongeza vifaa tiba lakini hajawaacha wananchi wa Kata ya Saranga.

Aidha, amemtaka fundi ujenzi aliyejenga kituo cha Afya cha mama na mtoto Mpiji Magoe kufanya marekebisho ya dosari alizozigundua mara moja kabla ya kumchukulia hatua za kumpeleka gerezani akajenge milango ya magereza.

"Ukiondoa taaluma yangu, pia ninauwelewa wa masuala ya ufundi, hivyo kwa kuangalia tu, yapo baadhi ya makosa ambayo tayari nimeelekeza uyafanyie kazi, nitarudi tena bila taarifa nikikuta hujarekebisha basi itabidi upelekwe gerezani maana kule kuna milango imeharibika"

Katika hatua nyengine  ametoa maagizo kwa Mamlaka ya Maji Safi na Mazingira (DAWASA) mkoani humo ambao umegharimu shill bill 36.8  kuanza mchakato wa kuzalisha umeme utakaotumika katika mashine za kusambazia maji ili kupunguza gharama.

Ameongeza kuwa, kwa sasa Dawasa inatumia bil. 2 kuilipa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) bil ya umeme, hivyo inaweza kuepuka gharama hiyo ikiwa itazalisha  umeme wake na Tanesco itumike kusambaza tu.

"Kuona mradi huu umeanza kufanya kazi , kwetu ni mafanikio makubwa na tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu.

"Hivyo huu si muda wa kudanyanyana kama sehemu kuna tatizo, kiongozi husika anatakiwa kusema ukweli ili Serikali itoe fedha, nikigundua kuna kiongozi hajasema ukweli kama kuna sehemu kuna tatizo ili wananchi wasaidiwe na nikabaini nitaanza na yeye," amesema.

Aidha, RC Chalamila ameagiza miradi yote iendane na thamani ya fedha unayotolewa katika Jimbo la Kibamba wilaya ya Ubungo na kuagiza miradi hiyo kujengwa kwa viwango na kuzingatia thamani ya fedha, ambapo ameagiza miradi hiyo kukamilika kwa wakati.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo,, Lazaro Twange, amesema kwamba kukamilika kwa mradi wa maji Kibamba  kutanufaisha kuondoa changamoto ya ukosefu ya maji katika Kata za jimbo hilo.

Pia Diwani wa Kata ya Kwembe, Nicolus Batiligaya amesema mwaka 2020,  kata yake ilikuwa na ukosefu wa maji na sasa wananchi wake wanapata huduma hiyo kwa asilimia 90.

"Natoa shukrani kwa Rais Samia kwa kutoa fedha kwa ajili ujenzi wa  miundombinu ya maji ambayo imeboresha maisha ya wananchi wangu kupata maji safi na salama na kuwepo utofauti mkubwa na miaka mitano iliyopita, " amesema.

Kwa upande wa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Juma Japhari Nyaigesha amewataka wananchi na wafanyabiashara kulipa kodi kwani ndio chanzo cha kupata fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo ikiwemo vituo vya afya huku Mganga Mfawidhi wa kituo cha Afya Mpiji Magoe Hereswida Cosmas akieleza maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo la mama na mtoto amesema ujenzi unaendelea vizuri na utakamilika kwa wakati.

Aidha Katika ziara hiyo wilayani Ubungo RC Chalamila pia ametembelea na kukagua mradi wa maji wa kibamba, pamoja na kukagua mradi wa shule ya sekondari goba kulangwa.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...