Skip to main content

TIMU YA YANGA YAKOSHWA NA "MAAJABU" YA TABORA ZOO





Pacome, Diarra wavutiwa na mnyama Simba

Na Beatus Maganja, TABORA 

 Viongozi na wachezaji wa Timu ya Young Africans (Yanga) leo hii wamefanya ziara katika Bustani ya Wanyamapori Hai Tabora, maarufu kama Tabora Zoo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kukuza utalii wa ndani na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini. Ziara hii iliongozwa na Rais wa Klabu ya Yanga, Injinia Hersi Said ikijumuisha wachezaji maarufu wa klabu hiyo.

Katika mazungumzo yake baada ya ziara, Injinia Hersi Said alisema kuwa lengo kuu la ziara hiyo ni kuonyesha mchango wa klabu ya Yanga katika kukuza utalii wa ndani na vilevile kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kutangaza vivutio vya utalii vya nchi yetu.  

“Ziara yetu hapa ni sehemu ya kuonyesha michango yetu katika kukuza utalii wa ndani, ikiwa ni njia mojawapo ya kuhamasisha Watanzania kutembelea vivutio vyetu vya utalii, lakini pia kuchangia uchumi wa taifa,” alieleza.

Katika kutekeleza dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kukuza utalii wa ndani, Rais wa Yanga alitoa wito kwa Watanzania, hasa wakazi wa Mkoa wa Tabora na mikoa jirani, kutembelea bustani hiyo ya wanyamapori ili kuendelea kuchangia uchumi wa Taifa kupitia utalii huku akisisitiza kuwa, Yanga, kama klabu kubwa ya soka nchini, ina nafasi ya pekee katika kutoa mchango mkubwa katika masuala ya kijamii na kiuchumi, ikiwa ni pamoja na kuhamasisha shughuli za utalii.

Hersi pia alitoa pongezi kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kwa juhudi zao katika kuboresha miundombinu ya utalii ndani ya bustani hiyo.

 Aliipongeza TAWA kwa kazi nzuri ya kuboresha mazingira ya hifadhi, akisema, “Pongezi kwa TAWA kwa mapokezi ya kipekee na huduma bora wanazozitoa. Maendeleo haya ni muhimu katika kukuza utalii wa ndani na kufanya vivutio vyetu kuwa vya kimataifa.”

Kwa upande wake, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Kanda ya Magharibi na Kaimu Kamanda wa Kanda hiyo, Wilbright Munuo, alieleza umuhimu wa Bustani ya Wanyamapori Hai Tabora katika kukuza utalii wa ndani. 

Munuo alisisitiza kuwa bustani hiyo ina mchango mkubwa katika kuhamasisha jamii kutunza rasilimali wanyamapori na kulinda mazingira. Alitoa wito kwa Watanzania kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha kuwa wanyamapori na mazingira yao vinahifadhiwa kwa manufaa ya taifa kwa ujumla. “Tunapaswa kuendelea kutunza wanyamapori wetu ili vizazi vijavyo vione na kufurahia rasilimali hizi. Hii ni sehemu ya kutimiza malengo ya kitaifa ya uhifadhi na maendeleo,” alisema.

Wachezaji wa Yanga pia walionyesha furaha yao kutokana na ziara hiyo na walieleza kufurahishwa na vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo katika bustani ya wanyamapori. Wachezaji maarufu kama Pacome, Diarra, Jonas Mkude, na Clement Mzize walionyesha kuvutiwa na mnyama Simba ambaye ni kivutio kikubwa katika hifadhi hiyo. Pacome na Diarra walieleza jinsi walivyovutiwa na mandhari ya hifadhi na wanyamapori waliokuwepo, huku wakiutaja mnyama Simba kama mmoja wa wanyama waliowavutia zaidi.

Ziara ya timu ya Yanga katika Bustani ya Wanyamapori Hai Tabora ilifanyika mara baada ya kumaliza mchezo wao wa ligi kuu dhidi ya Tabora United, ambapo Yanga ilishinda kwa mabao matatu kwa nunge.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...