Skip to main content

VIJANA WATAKIWA KUJITOKEZA KATIKA ZOEZI LA KUBORESHA DAFTARI LA MPIGA KURA

 


Na Mwandishi wetu 

Katibu wa Idara ya Chipukizi na Uhamasishaji wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Jesca Mshana, amewataka vijana wa kitanzania kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi la kuboresha daftari la kudumu la mpiga kura awamu ya pili, linalotarajiwa kuanza Mei 1 hadi 7, 2025.

Akizungumza na vyombo vya habari, Mshana amesema kuwa ni muhimu kwa vijana kutambua nafasi yao katika mustakabali wa taifa, kwa kuhakikisha wanajiandikisha ili wapate haki ya msingi ya kupiga kura.

Ameongeza "Kupiga kura ni haki ya msingi na sauti ya mabadiliko. Vijana msikose kushiriki kwenye hatua hii muhimu ya kidemokrasia,"

Ameleza kuwa mchakato huo utaanza katika mikoa ya Geita, Mwanza, Ruvuma, Mbeya na Songwe, kabla ya kuhamia kwenye mikoa mingine 16 ikiwemo Dar es Salaam, Arusha na Kilimanjaro. Vilevile, kuanzia Mei 16 hadi 22, uboreshaji utaendelea katika vyuo vya elimu ya juu pamoja na vituo vya magereza.

Aidha, Mshana amewataka vijana wajitokeze kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, akisisitiza kuwa taifa linahitaji fikra mpya na uongozi wenye dira kutoka kwa vijana.

"Tunahitaji mawazo mapya, vijana waonesheni uwezo wenu kwa kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali ili kubeba ajenda za maendeleo kwa vizazi vya sasa na vijavyo,"alieleza.

Hata hivyo, amewataka vijana kuwa uvivu wa kushiriki mchakato wa uchaguzi huacha nafasi kwa watu wasiokuwa na dhamira njema kuongoza taifa.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kudumisha amani ya taifa, akisema kuwa UVCCM na Chipukizi hawatakubali kuona amani ya nchi inavurugwa. 

"Tunaamini katika misingi imara ya waasisi wa taifa hili, na viongozi wa sasa wanaendeleza hilo, amani ni urithi wetu, na vijana tuna jukumu la kuilinda kwa gharama yoyote," 

Zoezi hilo la uboreshaji wa daftari ni sehemu ya maandalizi kuelekea uchaguzi mkuu, ambapo ushiriki wa vijana unaendelea kusisitizwa kama nguzo muhimu ya ujenzi wa taifa.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...