Skip to main content

WASIRA:CCM TUNAHUBIRI AMANI KWA SABABU NDANI YAKE KUNA HAKI




Asisitiza Chama hakiwezi kukubali mtu au kikundi cha watu kuvuruga amani iliyopo

Na Mwandishi Wetu, Tabora

MAKAMU Menyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Stephen Wasira, amesema ni vema wananchi wakafahamu kwamba katika amani ndani yake kuna haki, hivyo Chama kitaendelea kuihubiri kuhakikisha inapatikana haki.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mjini Dodoma alipokuwa akihitimisha ziara yake katika Mkoa wa Tabora, jana, Wasira amesema kuna watu wanahoji CCM inazungumzia sana amani lakini haizungumzii haki, huku akibainisha kuwa wanaotoa madai hayo  ni watu wazito.

“Sasa nikasema ngoja niende (Tabora) kwenye kitovu ambapo Mwalimu Julius Nyerere alitoa machozi kwa ajili ya amani, tuwasaidie kuelewa kwamba ukizungumza amani ndani ya amani kuna haki kwa sababu amani ikikosekana wenye uwezo mdogo wanaumia.

“Amani ikikosekana wanawake na watoto wao katika nchi jirani wanakilimbilia Tabora...ukilinda amani unalinda haki tena unalinda haki ya wanyonge, unalinda haki ya wasiokuwa na sauti.

“Unazungumza haki ya mtu anasema anataka kuwa Rais halafu anaambiwa eti tukibadili Katiba anakuwa Rais na haki inayosemwa ni mtu mmoja badala ya kuzungumza haki ya walio wengi. Tunauliza huyo anayesema hatuzungumzi haki tunazungumza amani sijui anadhani ndani ya amani hakuna haki.” Amesema Wasira.

Ameongeza kuwa kote ambako amani imekosekana haki ya wengi imepotea hususan nchi za jirani wananchi wake walikimbilia Tanzania, hivyo alihoji iwapo ikitokea amani iliyopo kukumbwa na dhoruba Watanzania watakimbilia wapi

“Wenyewe wamekimbia kwao na ninyi mnataka kukimbilia kwao mnapishana kama sisimizi. Hivyo tunasisitiza haki lakini haki iko ndani ya amani. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka vyombo na inasema kazi ya Bunge ni kutunga sheria, kazi ya Mahakama ni kutafsiri sheria na kuweka haki na haki hiyo ni haki ya kibinadamu, hatuzungumzi haki ya Mungu.

"Tumeweka mahakama kwamba ndio inayolinda haki za watu, sasa kama wewe unadhani hupewi haki uende kwenye mahakama ukadai hiyo haki yako usikilizwe ili ulete amani na upate haki yako kwa njia ya amani.

“Unatuambia utakinukisha, unatuambia utaichoma Tanzania nani anakupa leseni ya kuichoma Tanzania? Kwa idhini ya nani? Ndio maana tunawaambia wale wanaotaka kutumia nguvu tutawaambia hiyo sio njia halali unataka kuvunja haki ya wanyonge wa Watanzania

“Unataka kutengeneza matatizo yatakayofanya akinamama wakimbie kliniki na kliniki tulizowajengea zibomolewe kwa mabomu, hivyo hatuwezi kukubali hilo. Nawashangaa Watanzania ambao hawajaelewa na wakiwasikiliza wanawapigia makofi lakini hawajui gharama zake,” amesema Wasira.

Hivyo amewaambia wananchi kuwa ameamua kuwachochea Watanzania kupitia Tabora ambako ni chimbuko la amani iliyowekwa nchini kwa machozi ya Julius Nyerere kwamba amani hiyo lazima itadumu kwa gharama yoyote.

“Hatuwezi kuruhusu watu wachache au kikundi kinachotumwa na vibaraka na Wakoloni mambo leo kuja kuvuruga amani ya nchi yetu, hatutafanya hivyo. Narudia kuna amani na ndani ya amani kuna haki.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...