Skip to main content

KAFULILA AELEZA HOJA NZITO KUHUSU PPPC, KONGAMANO LAFANA








Na Mwandishi wetu 

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), David Kafulila amesema deni la dunia limekuwa likiongezeka ila deni la Taifa la Tanzania limebaki kuwa himilivu.

Aidha, Kupitia ( Public -Private Partnership ) PPP, Serikali inapunguza mzigo wa kifedha na kiutendaji huku ikihakikisha Miradi ya Maendeleo inakamilika kwa wakati.

Hayo ameyabainisha leo jijini Dar es Salaam wakati akiwasilisha mada katika Kongamano la kitaifa kuhusu ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi lenye mada kuu dola, masoko na uhamasishaji mitaji, nafasi ya Ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi kufikia malengo ya dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050.

Amesema kuwa,ongezeko la mahitaji ya rasilimali za kugharamia bajeti ya Serikali yamefanya dhana ya Ubia kati Sekta binafsi (PPPC) kugharamia miradi ya maendeleo kuwa na umuhimu wa kipekee nchini Tanzania.

Kafulila aliwasilisha mada inayosema nafasi ya PPP katika kufanikisha Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, ambapo amesema ni muhimu kuwa na PPP hasa katika ulimwengu wa sasa kwani kupitia PPP Miradi ya Maendeleo inakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa.

“Dhana ya PPP imelenga kuisaidia Serikali kukuza uchumi na kutoa huduma bora kwa wananchi”amesema Kafulila.

Ameongeza kuwa, PPP ni muhimu kwa ustawi wa Taifa si tu kusaidia kuvuta teknolojia mpya, bali pia kuleta ufanisi wa kiutendaji .

Kwa upande wake, mwanasiasa mkongwe nchini, Profesa Anna Tibaijuka akichagia mada iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa PPPDavid Kafulila amesema pesa hazitokani na Serikali, bali hutoka kwa wananchi ambao ndio chanzo kikuu cha rasilimali.

Amesema kuwa mfumo wa PPP ni nguzo muhimu kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 kwa kuwa unaleta uwazi na kuwahusisha wananchi moja kwa moja kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

"PPP siyo tu njia ya kuimarisha uchumi, bali ni utamaduni wa kushirikiana kwa uwazi, jambo linalowezesha miradi mikubwa kujadiliwa bungeni na kupewa kipaumbele"amesema

Naye Mhadhiri Mwandamizi kutoka Taasisi ya Uhasibu Arusha, Dkt. Kafigi Jeje ametoa wito kwa watendaji wa halmashauri zote nchini kuchukua hatua thabiti katika kusimamia miradi ya maendeleo kwa ufanisi.

Naye, Dkt Milanzi Mursali kutoka Tume ya mipango amesema kisheria ndio inajukumu la kuandaa dira na kwa Sasa wapo katika hatua za mwisho wa maaamuzi.

Aidha amesema kupitia dira ya 2050 inapenda kuona Serikali za mtaa zinafanya maamuzi pasipo kutegemea Serikali ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...