Skip to main content

MITAA 58 HALMASHAURI YA MJI WA TARIME IMEFIKIWA NA UMEME– MHE. KAPINGA


Ni kati ya mitaa 81 ya Halmashauri  ya Mji wa Tarime

Asema kazi ya kupeleka umeme vitongojini ni endelevu

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe Judith Kapinga amesema Serikali imefikisha  umeme kwenye mitaa 58 ya Mji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime kati ya mitaa 81 ya Halmashauri hiyo.

Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Mei 26, 2025 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la la Mbunge wa Tarime Mjini, Mhe. Michael Kembaki aliyeuliza Serikali itapeleka lini umeme katika mitaa 18 ya Halmashauri ya Mji wa Tarime. 

"Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ya Mji wa Tarime ina mitaa 81, kati ya hiyo mitaa 58 tayari  imefikiwa na umeme, na mitaa 23 bado haijafikiwa na umeme."  Amesema  Kapinga

Ameongeza kuwa, mitaa 13 inapelekewa umeme kupitia mradi wa Hamlets Electrification Project - IIA (HEP IIA) unaotekelezwa na Mkandarasi Dyname Construction Engineering,  na mitaa 10 iliyobaki itafikishiwa umeme katika miradi inayofuata.

Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Wanawake (UWT), Mhe. Zaytuni Swai aliyeuliza kuhusu jinsi  Serikali ilivyojipanga  kupeleka umeme maeneo ya pembezoni mwa mji wa Arusha hususan kwenye Kata ya Telat, Mhe. Kapinga ameeleza kuwa, Serikali inatekeleza miradi mbalimbali katika maeneo ya pembezoni  (Peri Urban)  kupitia Wakala wa Nishati Vijijini  (REA) ambayo lengo lake ni kusambaza  umeme maeneo ya pembezoni mwa mji.

Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Cecilia Pareso alyeuliza kuhusu Vitongoji vya Wilaya ya Karatu kutokuwa na umeme na vichache vilivyo kwenye mradi kupelekewa nguzo 40 ambazo hazitoshelezi mahutaji na kuiomba Serikali  kuongeza idadi hiyo, 

Kapinga amesema kuwa kwa kawaida miradi ya Vitongoji inawigo kulingana na kazi aliyopewa  Mkandarasi, hata hivyo amesema  kuwa Wilaya ya Karatu ipo katika mradi wa Vitongoji 9,000 ambao utaanza kutekelezwa hivi karibuni na kusisitiza kuwa, miradi ya kupeleka umeme kwenye Vitongoji ni endelevu.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...