Skip to main content

WAZIRI MCHENGERWA AFURAHISHWA NA UONGOZI WA MKOA WA DAR


Waziri wa Nchi  Ofisi ya Waziri Mkuu( TAMISEMI) Dkt, Mohamed Mchengerwa, ameupongeza uongozi wa mkoa wa Dar es Salaam chini ya mkuu wake Albert Chalamila kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kusimamia miradi ya maendeleo na utekelezaji wake .

Pongezi hizo alizitoa jijini Dar es Salaam katika kongamano la wamachinga wa Kariakoo la kumpongeza Rais Dkt Samia na kuliombea Taifa kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika hivi karibuni.

Amesema njia waliochagua wamachinga ndio sahihi ya kuleta maendeleo na kuisaidia Serikali inawaunga mkono ili waweze kuendelea kwani Taifa la Tanzania linaendelea kuwa salama na amani Rais wa JMT amefanya makubwa ikiwemo kuwashika wafanyabishara. 

Sambamba na hayo, ametoa maelekezo Wilaya ya Ilala kuhusu ujenzi wa Jangwani Mpya na majengo ya kisasa ya Wamachinga yaweze kuongezwa katika mji wa kisasa majengo ya wafanyabishara wamachinga yawekwe eneo hilo ujenzi ukikamilika waweze kutumia masoko na wao.

Akizungumzia masoko ya mkakati yatakayojengwa mikoa yote pia wamachinga wapewe kipaumbele sekta hiyo muhimu ya wafanyabishara nchini.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa wowote kutokana na jitihada zake za utendaji kazi katika juhudi za kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan. 

"Katika wakuu wa wilaya wanaofanya kazi na kujituma Mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo anafaa kuwa mkuu wa mkoa wowote kutokana na ufanyaji kazi wake katika kuisaidia Serikali ya Tanzania ya Dkt.Samia Suluhu Hassan ,ameweza kumsaidia Rais, ambapo pia katika wakuu wa Wilaya Tanzania Edward Mpogolo anashika namba moja anajishusha kwa jamii "amesema Waziri  Mchengerwa. 

Waziri Mchengerwa amesema Viongozi wa wilaya ya Ilala wanafanya kazi nzuri kwa kushirikiana pamoja na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu wamepata Mbunge makini kwa kuchapa kazi kwa maslahi ya Ilala na Taifa kwa ujumla.

Katika hatua nyingine amemwagiza Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam Albert John Chalamila aendelee kufanya kazi kwa weledi na kuakikisha Dar es Salaam inakuwa kitovu cha amani katika kipindi chote.

Kwa upande wake, Mkuu wa  Mkoa Dar es Salaam Albert John Chalamila alizungumzia mgogoro wa Wafanyabishara Wenye Asili ya Wachina alisema changamoto hiyo inaitaji ustarabu utumike na Demokrasia watakaa na kikao na Waziri wa Viwanda Selemani Jafo kwajili ya kumaliza mgogoro huo uliojitokeza na wafanyabishara wa Tanzania. 

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo alimpongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa Ilani ya chama kwa kutoa zaidi ya bilioni 300 za miradi mbali mbali ya maendeleo ya sekta ya Elimu, afya na miundombinu ya barabara. 

Akizungumzia Wamachinga wa wilaya ya Ilala alisema hivi karibuni Rais atajenga soko la machinga la lisasa hivyo wafanyabishara waendelee kufurahia matunda ya Serikali yetu ya awamu ya sita  

Hata hivyo, amesema mikopo ya asilimia kumi ambayo inatolewa ngazi ya Halmashauri alisema mikopo yote itaenda kwa wafanyabishara vikundi vyote vilivyosajiliwa ambavyo vimeomba mikopo ya Serikali na kutimiza taratibu .

Mbunge wa jimbo la Ilala Mussa Zungu ambaye ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alisema mikakati ya Rais kila mtu afanye shughuli zake kwa Amani na mambo makubwa yanakuja ya Serikali ya Dkt.Samia ambapo alitumia nafasi hiyo kuwapongeza wafanyabishara Wamachinga kwa kufanya Kongamano kubwa hilo huku aliwataka wajiandae mwezi Octoba kumpigia kura Rais Dkt.Samia kwa wingi .

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...