Skip to main content

WAZIRI MCHENGERWA AMPA TANO KUMBILAMOTO


Na Mwandishi wetu

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya waziri mkuu (TAMISEMI) Dkt Mohamed Mchengerwa, amemtabiriwa mambo makubwa Meya wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto, ambaye ni Diwani wa kata ya Vingunguti kwa utendaji bora wa kazi katika kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Aidha, Waziri Dkt Mohamed Mchengerwa  amesema hayo wakati wa kuzindua mradi wa Serikali wa ujenzi wa soko la nyama  choma la lililopewa jina la KUMBILAMOTO mradi huo uliopo machinjio ya Vingunguti wilayani Ilala. 

"Nawapongeza Madiwani wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam mmepata Meya bora Omary Kumbilamoto, mchapa kazi na anafanya kazi kwa weledi za Serikali anajua kazi yake isingekuwa katiba ya chama cha Mapinduzi Meya Omary Kumbilamoto  anapita bila kupingwa na Jimbo lingegawanywa angepewa jimbo moja  "amessema Dkt Mchengerwa. 

Amesema kuwa, kutokana na utendaji kazi wa Meya Kumbilamoto ni vyema madiwani wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kumpa ushirikian  katika kumsaidi Rais Dkt.Samia  Suluhu Hassan na kusimamia miradi ya maendeleo  vizuri ya Halmashauri. 

Wakati huohuo alitoa agizo sheria ibadilishwe Naibu Meya wa Halmashauri achaguliwe kila baada miaka mitano kuanzia sasa sio mwaka mmoja ili kuondoa migogoro ndani ya chama cha Mapinduzi CCM. 

Hata hivyo, amemwagiza Katibu Mkuu TAMISEMI kuwasilisha kanuni haraka Bungeni ili aweze kusaini kurekebisha kabla Bunge la Jamhuri ya Muungano kuvunjwa ili iweze kutumika haraka  .

Kwa upande mwingine alimwagia sifa Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Elihuruma Maberya anafanya kazi kubwa katika Wakurugenzi 184 nchini Mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam ameshika namba moja anafanya kazi kubwa ya kumsaidia Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kukusanya mapato mengi na kuvunja rekodi. 

Akizungumzia suala la amani ya nchi alimwagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kuwakamata wote wanaovuruga anani ya nchi yetu kwani katika suala la amani uwezi kuzungumza ukajificha tuilinde amani kwa nguvu zote kwani inapotokea machafuko uwezi kuangalia mzee au kijana.

Kwa upande wake Meya Kumbilamoto, amesema dhumuni la kujenga mradi huo wa nyama choma wafanyabishara waliandamana nyumbani kwake  ambapo awali kulienea uvumi eneo hilo la Serikali limeuzwa ambapo taarifa sio za kweli leo mradi wa Serikali umekamilika uliogharimu shilingi bilioni 729.6 fedha zilizotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri. 

Meya Kumbilamoto amesema katika mradi huo wa ujenzi wa jengo la soko la nyama choma la Kumbilamoto watafunga TV kubwa za kisasa kwa ajili ya Wananchi waweze kufatilia matukio mbali mbali ikiwemo taarifa ya habari.

Akizungumzia maendeleo ya Serikali kata ya Vingunguti ameweza pia kusimamia DAWASA wananchi wanapata maji safi na salama, sekta ya  elimu NMB na Serikali ya Dkt.Samia imeweza kuleta madawati ya kutosha wanafunzi wanakalia madawati na shilingi milioni 700 Rais ameleta kwa ajili ya sekta ya elimu pia

Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Elihuruma Maberya ,alisema katika soko hilo la nyama choma Vingunguti kutakuwa na huduma za kifedha ambapo alimpongeza Meya kwa kuizinisha mradi huo wa maendeleo Halmashauri hiyo itasimamia kuwawezesha wajasiriamali wadogo kukuza uchumi wa nchi yetu .

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...