Skip to main content

DKT. BITEKO AZIPONGEZA SSF NA TOTAL ENERGIES KUFIKIA VIWANGO VYA JUU VYA USALAMA VYA USAFIRISHAJI









Asema Serikali inaweka sera za kulinda na kuvutia wawekezaji

Wenye malori watakiwa kuweka vifaa vya usalama

Rais Samia apongezwa kwa kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji nchini

 Wasafirishaji watakiwa kuzingatia usalama barabarani

Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amezipongeza Kampuni za Total Ernergies na Super Star Fowarders – SSF  kwa kuweza kufikia viwango vya juu vya usalama vya usafirishaji huku akiwataka wasafirishaji wengine kufuata  nyayo zao kwa kuwa kampuni hizo ni mfano mzuri wa kuigwa.

Dkt. Biteko amesema hayo Juni 25, 2025 jijini Dar es salaam wakati akishiriki katika maadhimisho ya miaka 30 ya ushirikiano kati ya Kampuni ya Super Star Fowarders (SSF) na Total Energies.

  “ Leo tumekusanyika hapa kusherehekea hafla ya miaka 30 ya ushirikiano baina ya Kampuni zetu hizi mbili za Total Ernergies na Super Star Fowarders. Katika kipindi hicho chote, mmekuwa washirika wakubwa wa kimataifa katika usafirishaji wa bidhaa mbalimbali hususan kwa kutumia matenki maalum, hakika, binafsi nimefarijika sana  na hongereni sana” amesema Dkt. Biteko.

Amesema kupitia ushirikiano huo umewezesha  upatikanaji wa uhakika wa mafuta nchini na kutoa ajira kwa mamia ya vijana pamoja na  kuvutia nchi za jirani kutumia Bandari ya Dar Es Salaam kupitishia mizigo yao na kutoa fursa kwa Watanzania. 

Ametoa wito kwa wasafirishaji wote wa mizigo kwa kutumia malori nchini wazingatie viwango  vya juu vya  usalama barabarani kwa kuhakikisha malori yao  yanawekwa vifaa vyote vya usalama kama vile GPS kufuata miongozoi liyopo. 

Fauka ya hayo, Dkt. Biteko amewahakikishia kuwa Serikali itaendelea kushirikiana kwa karibu na wafanyabiashara wote na kuwatengenezea mazingira mazuri ya kazi ikiwa ni pamoja na kuweka sera zenye kutabirika ambazo zitawalinda na kuvutia wawekezaji zaidi nchini.

Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amewataka wasafirishaji kuzingatia usalama barabarani kwa kuwa suala hilo sio sera tu bali ni kwa maslahi mapana ya Taifa na  ajali za barabarani zinasababisha hasara kubwa ikiwemo uhai wa watu na uchumi wa nchi. Aidha, ametoa wito kwa wasafirishaji nchini kutumia barabara zilizopo kwa kuzingatia viwango.

Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Anne Sophie amesema siku hiyo ni muhimu kwa Tanzania na Ufaransa kwa kuadhimisha miaka 30  ya  ushirikiano kati ya kampuni hizo mbili ambao umekuwa na faida akitolea mfano mafunzo kwa madereva na matumizi ya  vifaa na mifumo ya kuzingatia usalama barabarani.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa  Kampuni ya Super Star Fowarders (SFF), Bw. Seif  A. Seif amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake na jitihada zinazosaidia kuimarisha na kukuza sekta ya usafirishaji nchini.

Kwa upande wake, Makamu wa Rais Mwandamizi wa  Kampuni ya Total Energies Kanda ya Afrika – Huduma za Masoko, Bw. Jean Phillipe Torres ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na dhamira yake katika kuimarisha sekta ya nishati nchini.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...