Skip to main content

RAIS SAMIA ATAJA MAFANIKIO SEKTA YA NISHATI 2020-2025







Ni wakati akihitimisha shughuli za Bunge jijini Dodoma

JNHPP, Umeme Vijijini, Umeme wa Gridi Kigoma na  Katavi; Ni baadhi ya Vielelezo vya mafanikio

Ataja miradi mikubwa ya usafirishaji umeme iliyokamilika

Ataka TANESCO  kuanza kuiangalia  Nyukilia kama moja ya vyanzo vya kuzalisha umeme nchini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameeleza kuwa Sekta ya Nishati imekuwa na mafanikio makubwa  katika kipindi cha miaka mitano. 

Ameyasema hayo wakati akihitimisha shughuli za Bunge Jijini Dodoma tarehe  28 Juni 2025.

"Mheshimiwa Spika kutokana na umuhimu wa Sekta ya Nishati kwa maendeleo ya nchi, Serikali imeimarisha upatikanaji wa nishati nchini ikiwemo kukamilisha mradi wa bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere (JNHPP)”. Amesema Mhe. Samia

Ameongeza kuwa, mbali ya kukamirisha mradi wa Julius Nyerere pia Serikali imekamilisha upelekaji wa umeme katika Vijiji vyote 12,318  nchini.

Ameongeza kuwa, msukumo uliofanywa na Serikali katika sekta ya nishati umewezesha uzalishaji wa umeme kuongezeka hadi kufikia megawati 4031.71 kutoka megawati 1,601.84 mwaka 2020.

"Hali hii imechangiwa na miradi mbalimbali ya uzalishaji umeme ukiwemo mradi wa kielelezo wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere wenye megawati 2115, vilevile mradi wa Kinyerezi I Extension wa megawati 185 na mradi wa Rusumo ambao tumeutekeleza kwa ushirikiano wa Nchi tatu za Tanzania, Burundi na Rwanda kwa mgawanyo wa megawati 26.67 kwa kila Nchi”. Amesema Rais Samia

Katika miradi ya usafirishaji umeme amesema Serikali imekamilisha miradi ya usafirishaji umeme ya kutoka Singida hadi Arusha, Geita hadi Nyakanazi, na Julius Nyerere hadi Chalinze.

Miradi mingine ni Nyakanazi hadi Kigoma, Tabora hadi Urambo, Rusumo hadi Nyakanazi na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kwenye njia ya Reli.

Amesema mafanikio hayo yameongeza upatikanaji wa umeme wa uhakika katika maeneo mbalimbali nchini.

Aidha ameeleza kuwa,  Serikali imefanikiwa kuiunganisha mikoa ya Kigoma na Katavi na gridi ya Taifa.

Kuhusu umeme Vijijini, Rais Samia amesema Tanzania imefikia hatua kubwa na ya kihistoria kwa kuunganisha Vijiji vyote 12,318 vya Tanzania Bara na huduma ya umeme.

Amesisitiza kuwa, kwa sasa Serikali inapeleka umeme kwenye Vitongoji ambapo vitongoji 33,657 tayari vimeshafikishiwa umeme kati ya Vitongoji 64,359 sawa na asilimia 52.3.

Kuhusu nishati mbadala, amesema Serikali inampango wa kuzalisha nishati mbadala kwa kutumia vyanzo jadidifu ambapo amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO kuanza kufikiria kuanza kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya Nyukilia.

Katika hatua nyingine, Rais Samia amesema  Serikali inapanga kuweka ushindani katika Sekta ya nishati kwa kuialika sekta binafsi kushiriki kuongeza upatikanaji wa umeme.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...