Skip to main content

WANAOTAKA KUHARIBU UCHAGUZI MKUU WAONYWA, VIJANA WA CCM WACHARUKA



Na Mwandishi wetu

Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam wamewaonya wanasiasa na wanaharakati wanaohamasisha wananchi wasishiriki Uchaguzi Mkuu kwani ni dai la kikatiba na sio matakwa ya mtu binafsi.

Akizungumza na  Waandishi wa habari Makao Makuu ya UVCCM Jijini Dar es salaam,mmoja wa Vijana hao Isack Sumbali amesema kuwa mabadiliko ya Sheria ya Uchaguzi yamefanyika kwa kiasi kikubwa ikiwemo Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) kubadilishwa nakuwa Tume huru ya Taifa ya  Uchaguzi(INEC).

Amesema kuwa, tume miongoni mwa mabadiliko ni pamoja na kua na uhuru wa vyanzo vya mapato, ambapo awali ilikua haiwezi kujiendesha kwa fedha za ndani,na kutegemea ufadhili kutoka UNDP, ambapo uchaguzi mkuu wa mwaka huu utagharamiwa na fedha za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha Sumbali amesema kuwa kwa sasa Uhuru wa Tume hiyo umeongezeka katika sehemu kuu mbili ambazo ni uhuru wa kitaasisi na uhuru wa kiutendaji,pamoja na kutungwa Sheria maalumu inayoongoza kupatikana kwa wajumbe wa tume tofauti na hapo awali wajumbe hao walikua wakiteuliwa na Rais.

Amongeza kuwa, mwaka huu kwa mara ya kwanza wafungwa waliopo Magerezani  watapiga kura,hapo awali wafungwa Magerezani walikua hawafikiwi kujiandikisha kupiga kura,jambo ambalo linatokana na INEC kupewa  uhuru mkubwa.

"Mabadiliko mengine ni kudhibitiwa kwa unyanyasaji wa kijinsia kipind Cha uchaguzi,matumizi ya teknolojia wakati wa uboreshaji wa taarifa za mpiga kura,hivyo kupitia mabadiliko hayo uchaguzi utafanyika na pasitokee upotoshaji wa aina yoyote kuwa uchaguzi hautafanyika,kwani Serikali imefanya mabadiliko hayo ili kufanya Uchaguzi uwe wa haki."amesisitiza 

Nae Antipas Pamba amesema kuwa yapo maeneo mahususi ambayo Serikali imeamua kugusa uchumi wa wananchi wa kawaida pamoja na Vijana,kuhakikisha inaweka mazingira rafiki kwa ajili ya kufanya shughuli za kiuchumi.

"Serikali imeendelea kutoa ruzuku kwa kaya masikini,takribani shilingi bilioni 961.5 zimetolewa kwa watu wa kawaida wasiojiweza,pia Serikali imegharamia mpango wa Elimu bila ada kuanzia shule ya Msingi hadi kidato cha sita ambapo shilingi trioni 1.3 zimetumika katika mpango huo.

Ameongeza kuwa, takwimu za Sensa ya Watu na Makazi zinaonesha asilimia 70 ya wakazi Nchini Tanzania ni Vijana hivyo kila jambo ambalo Serikali inalitekeleza wanufaika wakubwa wa jambo hilo ni Vijana.

Aidha amesema kuwa Serikali imeendelea kutoa Mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu na Vyuo vya kati,hadi sasa kiasi cha shilingi trioni 2.7 zimetumika katika mpango huo wa kusomesha watoto wenye hali ya maisha ya chini,pamoja na kutumia kiasi cha shilingi bilioni 709 kwa ajili ya kutoa ruzuku ya mbolea kwa Wakulima.

Nae, Mabula Marco Mabula amewaomba Vijana wajitokeze kwa wingi kuchukua fomu za kugombea nafasi za Udiwani na Ubunge pamoja na kumpigia kura Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(CCM),Dkt.Samia Suluhu Hassan.

"Kwa Vijana wa CCM watakaojitokeza kungombea nafasi hizo,chama chao kimewatengenezea utaratibu mzuri wa kushiriki nakuhakikisha wenye uwezo na sifa za kuongoza wanashinda"

Ameongeza kuwa " miaka ya nyuma watu walikua wana nunua hizo nafasi,unakuta mtu anafedha anawahesabu kama njugu anawapa fedha,lakini chama chetu kimesema huo utaratibu hapana maana yake huwezi ukahonga zaidi ya watu elfu nane,hii ni hatua kubwa sana iliyofanywa na chama chetu".

Mabula amesema kuwa Chama Cha  Mapinduzi hakiko tayari kuachia nchi kwasababu wananchi wanaona maendeleo yaliyofanywa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye ametekeleza Ilani ya CCM kwa zaidi ya asilimia 95.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...